BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKURUGENZI WA RAIS MAGUFULI AKOSA SIFA YA KUWA MKURUGENZI HALMASHAURI YA RUNGWE MBEYA ?


Wakurugenzi wakila kiapo Ikulu.Picha ya Maktaba

Dar.
Ukihukumiwa na mahakama ama kwenda jela au kulipa faini, unapotekeleza adhabu mojawapo bila kuikatia rufani ni wazi unakubaliana na makosa, hali hiyo ndio inayomkuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe mkoani Mbeya, Loema Isaya Peter aliyeteuliwa na Rais Magufuli hivi karibuni.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama na kuthibitishwa na mwenyewe (Loema), alipatikana na hatia kwa makosa ya jinai akiwa mtumishi wa umma.

Loema, ambaye aliwahi kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM lakini akaanguka, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya Sh500,000 kwa kosa la kutumia vibaya madaraka. 


Alilipa faini na hakukata rufaa kwenye hukumu ilitolewa mwaka jana, hivyo kumfanya apoteze sifa ya kuajiriwa tena kwenye utumishi wa umma. 

Akiwa anakaimu nafasi ya ofisa utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Loema alishtakiwa na Takukuru kwa kushirikiana na ofisa mwenzake anayeitwa Kabubi Mmbondo, kumuajiri mtu ambaye hakuwa na sifa na kumuacha aliyestahili.CHANZO/MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: