BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIGI DARAJA LA KWANZA NETIBOLI TANZANIA BARA, POLISI MOROGORO YATIMUA VUMBI.

Mchezaji wa timu ya netiboli ya Madini ya Arusha akichuana na Demetria Sadala wa Polisi Arusha wakati wa ligi daraja la kwanza mchezo wa netiboli Tanzania bara inayofanyika kwenye uwanja wa ndani wa jamhuri Morogoro, Polisi Arusha ilikubali kufungwa vikapu 62-48.PICHA/JUMA MTANDA.
 
Juma Mtanda, jphtjuma@gmail.com
Ligi daraja la kwanza mchezo wa netiboli Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 imeanza kutimua vumbi huku timu wenyeji za Polisi Morogoro na Tumbaku zikianza vyema ligi hiyo kwa kupata ushindi mnono katika michezo yao ya kwanza mbele ya wapinzani wao katika uwanja wa ndani wa jamhuri mkoani Morogoro.

Timu ya Polisi Morogoro ilianza kutupa karata yake dhidi ya Tanga jiji na kuibuka na ushindi wa vikapu 85-12 huku Tumbaku yenyewe ikipata ushindi kwa kuilaza Kinondoni ya Dar es Salaam kwa vikapu 90-17.

Timu ya Polisi Morogoro iliendelea kasi yake baada ya kupata ushindi mwingine kwa kuiadhibu Kinondoni ya Dar es Salaam vikapu 88-13 huku Tumbaku ya Morogoro ikiteleza kwa kufungwa vikapu 62-32 na mabingwa watetezi timu ya Uhamiaji.

Katika michezo mingine, Jeshi Stars ilipata ushindi kwa kuilaza Ras Kagera kwa vikapu 89-18 huku CMTU ya Dar es Salaam ikiambulia kipigo cha vikapu 46-42 kutoka kwa Arusha Quens huku Arusha City ikitoshana nguvu na Madini ya Arusha kwa kufungana vikapu 36-36.

Jeshi Stars iliinyanyasa Polisi Arusha kwa kuitandika vikapu 64-38 wakati Ras Kagera ilikiona cha mtema kuni mbele ya timu ya CMTU kwa vikapu 88-13 na Madini Arusha ilipata ushindi mbele ya Polisi Arusha wa vikapu 62-48.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira alieleza kuwa mashindano ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya timu 11.

Kibira alieleza kuwa ligi hiyo imeanza kuchezwa tangu Agosti 27, mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri wa Morogoro ikishirikisha weenyeji timu, Polisi Morogoro, Tumbaku Morogoro, Madini Arusha, Jiji Arusha, Polisi Arusha, Kinondoni, Ras Kagera, Jeshi Stars, Jiji Tanga na mabingwa watetezi timu ya Uhamiaji.

Ligi hiyo inatarajia kumalizika septemba 4 mwaka huu.Chanzo/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: