ASKARI NA SILAHA.
Mapigano makali yaliyotolea leo kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani yamesababisha kifo cha askari wa ngazi ya juu.
Timu ya Mwananchi ambayo iliweka kambi eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (difenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yaliyokuwa yanakwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru njia zilifungwa kutokana na mapambano hayo.
Inadaiwa kuwa majambazi 14 yamekamatwa huku wengi wao wakidaiwa kuwa ni askari wastaafu akiwemo Kiongozi wa wahalifu wao anadaiwa kuwa ni Kanali wa Jeshi mstaafu.
Polisi iliweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, Mkuranga huku magari yote yaliyokuwa yanatoka na kuingia Dar yakiwa yamezuiliwa.
Aliyefaeiki dunia katika tukio hilo ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Majambazi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Thomas Njiku ambaye alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi ya kichwa katika maeneo ya Vikindu Mkoani Pwani na watu wanaosadikika kuwa ni magaidi.
Nyumba inayodaiwa kuishi majambazi hayo ikiwa imechakazwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ POLISI APIGWA RISASI NA KUFARIKI NA MAJAMBAZI YAKIPAMBANA NA POLISI MKURANGA, PWANI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment