NAIBUKA KATIBU MKUU CUF TANZANIA BARA AMCHOKA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD SAKATA LA PROF LIPUMBA.
Taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii juu ya mgogoro ulioibuka ndani ya CUF unaendelea kuibua mapya.
Chini ni maelezo yanayodaaiwa kuandikwa na Naibu Katibu kuu wa chama cha wananchi CUF Tanzania bara, Magdalena Sakaya (MB) juu ya kuelezea chanzo cha kuvunjika kwa mkutano mkuu maalumu hivi karibuni na hiki ndicho kinachodaiwa kuandikwa na mheshimiwa Sakaya.
"Niko tayari kufukuzwa, ila sitonyamaza wala kubadili msimamo wangu, CUF ni TAASISI si KAMPUNI na Cuf sikuletwa na mtu, Cuf si maisha yangu, Cuf hawaninyimi pumzi, watafukuza wengi kama hawataki kufuata Katiba. ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Na kuendelea kueleza kuwa, Sio siri mimi ni Naibu Katibu Mkuu ; wajumbe FEKI waliingizwa kwa usimamizi wa Katibu Mkuu , Seif Shariff Hamad . CUF kuna mgogoro mkubwa ambao Katibu Mkuu , anatumia kila njia wanachama wasiujue na hataki kabisa usemwe wazi.
Profesa Lipumba , ni kipenzi cha watu wengi ; kulazimisha kumuondoa kwa hoja za ujanjaujanja , ni kukiweka Chama katika hali tete sana . CUF kuna mpasuko mkubwa , ambao hauzungumzwi ukaeleweka .
Kuna SIRI NZITO na mambo ya ajabu sana . Nashangaa kwanini Katibu Mkuu wangu anashindwa kukubali kumaliza mgogoro huu kwa amani , au kuweka wazi jamii ijue ! ! Ni kusoma tu alama za nyakati , kwamba Watanzania bara sasa wameamka ; kuendelea kuwaburuza ni kujidanganya.
Niko tayari kwa maamuzi yoyote ya kunifukuza , lakini sitokubali msimamo wangu wa kutaka Katiba ufuatwe . MAAMUZI ya kukubali kujiuzulu Profesa Lipumba , au la bado hayajafanyika.
Lazima Mkutano Mkuu ukutane na uamue , kuhusu barua ya kujiuzulu pamoja na barua ya kutengua . Na sio kusoma barua moja tu ya kujiuzulu , tena kwa ujanjaujanja. ilimaliza taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment