Na Buberwa Jackob.
Wanachi Tusikubali kufanywa chambo cha kuvunja amani tuliyoijenga
Wasanii wa kitanzania wanaoishi na kufanyia kazi zao nje ya nchi au ughaibuni,wametoa wito kwa wananchi wa Tanzania walio nyumbani na nje kupinga kwa nguvu zote maandamano yaliyopewa na jina la UKUTA yalipangwa kufanyika siku 1 september 2016.
Wasanii hao wakikaliliwa na vyombo vya habari walisema maandamano hayo hayana tija kwa watanzania na zaidi yataleta mpasuko katika jamii.
baadhi ya wasanii hao ni mwanamuziki Saidi Kanda anayeishi nchi uingerea alisema " Hakuna haja ya Kuunga mokono maandamano yatakayo lisababishia taifa uvunjifu wa amani" baadala yake wanasiasa watuache wananchi tufanye shughuli zetu na kufurahia maisha- Alisema mwanamuziki Saidi Kanda kiongozi wa Mvula-Mandondo Band ya Uingereza.
Kule Ujerumani nako Kiongozi wa Ngoma Africa band mwanamuziki maarufu Kamanda Ras Makunja alikuwa akiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya wasanii waishio ujerumani ambapo mtazamo wa Kamanda Ras Makunja una hoja nzito kuhusu maandamano ya UKUTA.
Watanzania tusikubali kufanywa mtaji au chanzo cha vurugu na uvunjivu wa Amani ambayo kwa miaka tumeijenga, kwani hatuoni sababu yeyote ya msingi ya kuunga mkono maandamano ya UKUTA.
Sisi watanzania ndio tuliopiga kula kuiweka serekali ya awamu ya tano,leo hii heti tuende mtaani kuandamana kuipinga !? kwa sababu ya watu wanajiita UKUTA kwa kweli itakuwa sawa na watoto walio juu ya tawi la mti na kuanza kulikata tawi walio kalia kwa shoka ni sawa Ukichaa- Ras Makunja alihoji.
Mwanamuziki huyo nguli alizidi kuhoji hivi wanasiasa si tuliwapa muda wa kutushawishi kuwapigia kura katika kampeni zao na sasa uchaguzi umepita.
Kuna haja gani tena sisi raia tushawishiwe kuandamana maandamano ambayo tafsiri yake UKUTA kisheria hayakubaliki yaani ukiyatazama kwa upana haya nia ya AMANI !.
Yaani mfano wake yawe maandamano kama ya
IRANI yalioshawishiwa kumtoa Shah ? lakini Tanzania sio Irani kwa sababu serekali ya Tanzania imechaguliwa na wananchi kihalali sasa leo sisi wapiga kura tena tuende mtaani kupinga kitu ambacho tumekichagua kihalali..? .
SHAH wa Iran alikuwa mfalme sio kiongozi wa kuchaguliwa ndio maana Khomen alishawishi wanafunzi waanze kuandamana, Maandamano ya India 1947 yakiongozwa na Ghandi yalikuwa ya kumuondoa mkoloni mwingereza,Sasa haya ya UKUTA na tafisiri yake ipo wazi ni yanini? .
kwa faida zipi za taifa letu,TUNAWAOMBA WANANCHI TUSIKUBALI KABISA KUUNGA MKONO MAANDAMANO YA UKUTA, tusikubali kushawishiwa kuandamana kwa madai yasiyoleta maandeleo kwa taifa, tusikubali kila siku.
Baadhi ya wanasiasa wanatuendesha mara tususie kupiga kura, mara tuandamane UKUTA wakati nchi jirani wanachapa kazi sisi tupo katika siasa kila kukicha ?! Ras Makunja alisisitiza kuwa anayo haki ya kutoa maoni yake kwani yeye bado raia halali wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment