BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIWANI WA CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA AMA KUMLIPA FIDIA POLISI SH 1.3 MIL MOSHI


Moshi. Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Kilimanjaro, imemtia hatiani Diwani wa kata ya Pasua mjini Moshi kwa tiketi ya Chadema, Charles Mkalakala (47) kwa makosa mawili likiwamo la kumshambulia Polisi.

Mbali na kumtia hatiani kwa kosa hilo, lakini mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo pia ilimtia hatiani diwani huyo na washirika wake wengine watatu kwa kosa lingine la kumzuia polisi huyo kufanya kazi yake.

Hukumu hiyo ilitolewa jana ambapo kwa kosa la kumshambulia Polisi huyo, Diwani huyo alihukumiwa kulipa faini ya Sh 500,000 na kumlipa polisi huyo fidia ya Sh 400,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela. 


Katika kosa la pili lililomhusisha Diwani huyo na washitakiwa, Hussein Mkalakala (21), Fikra Said (23) na Raymond Andrea(34), Mahakama iliwahukumu kulipa faini ya Sh400,000 kila mmoja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: