Juma Mtanda, Morogoro-jphtjuma@gmail.com
Kaya zaidi ya 300 zenye wakazi 1767 katika kijiji
cha Ngaite kata ya Parakuyo wamekumbwa na wasiwasi na hofu baada ya diwani wa
kata hiyo, Ibrahim Oloishuro Kalaita kuitisha mkutano wa kijiji na kuwasilisha
pendekezo la kufutwa kwa kijiji hicho kutokana na sababu mbalimbali wilaya ya
Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika shule ya
msingi Ngaite jana, Oloishuro Kalaita alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya
Kilosa kupitia idara ya ardhi na maliasili imetoa pendekezo la kufutwa kwa
kijiji hicho jambo lililopelekea wananchi hao kukumbwa na mshtuko na wasiwasi
wa namna ya kuanza maisha mapya.
“Niliagiza viongozi wa kijiji waitishe mkutano mkuu
wa kijiji kisha waeleze sababu za pendekezo la kufutwa kwa kijiji la Ngaite
lililopendekezwa na halmashauri ya wilaya ya Kilosa kupitia idara ya ardhi na
maliasili lakini mapokeo yamekuwa tofauti na kuzua hofu na wasiwasi mkubwa juu
ya maisha yao.”alisema Oloishuro Kalaita.
Jana (Juzi) nilifanya mkutano wa kijiji wa
ufafanuazi juu ya pendekezo hilo lakini mwitikio wa wananchi hao juu ya jambo
hilo bado umeendelea kukubikwa na hofu.
wakizungumza katika mkutano huo, Christina Kiamba (49)
na Elizaberth Changalima (61) walisema kuwa wamestushwa na taarifa ya pendekezo
la kufutwa kwa kijiji cha Ngaite kutokana na uwepo wa kuimarika kwa huduma za
jamii ikiwemo shule.
“Ngaite tayari imekuwa na maendeleo na ina jamii
kubwa sasa kama kijiji kitafutwa jamii hii yenye kila aina ya rika serikali
itaipeleka wapi ?...tumeambiwa na viongozi wetu mipango iliyopo ni kuimarisha
miundombinu ya barabara na ujenzi wa jengo la zahanati.”alisema Chritina.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Kilosa, Kessy Mkambala akitoa ufafanuzi juu ya pendekezo la halmashauri yake
kupitia idara ya ardhi na maliasili kufutwa kwa kijiji cha Ngaite alisema kuwa wananchi
wa kijiji hicho wasipatwe na hofu.
Mkambala alisema kuwa kijiji cha Ngaite hakitafutwa
na wananchi wataendelea kuishi eneo hilo isipokuwa mamlaka ya kijiji hicho ndio
yatafutwa na mamlaka yatakuwa katika kijiji mama cha Malangali kata ya tarafa.
“Halmashauri imetoa mapendekezo kupitia watalaamu la
kufutwa kwa mamlaka ya kijiji cha Ngaite na mapendekezo hayo yatapishwa na
baraza la madiwani kama wataridhia pendekezo hilo ama kukataa.”alisema
Mkambala.
Mkambala alisema kuwa moja ya sababu za pendekozo la
kufutiwa kwa mamlaka ya kijiji cha Ngaite ni pamoja na mchakato wa kuanzisha
kijiji cha Ngaite haukuzingatia taratibu zote za kisheria ya serikali za mitaa
namba 7 ya 1982 (sura ya 289/2002).
Sheria ya ardhi namba 5 1999 inazitaka vijiji kuwa
na kaya zisizopungu 250 nna kuwa na eneo ambalo mipaka yake
inatambulika.alisema Mkambala.
Aliongeza sababu nyingine kuwa ni kijiji kuwa na
eneo la kutosha la shughuli za kiuchumi na jamii za sasa na za baadaye pamoja
na njia za mawasiliano hususani barabarani.
“Kijiji chote cha Ngaite kipo ndani ya shamba la
mifugo la Narco lenye hatimiliki hivyo kusababisha kijiji kutokuwa na ardhi hata
kijiji hicho kinaanzishwa kamati ya maendeleo ya kata husika hakuidhinishwa na
kata husika maombi ya kuwa kijiji.”alisema Mkambala.
Kijiji cha Ngaite ni miongoni mwa vijiji vitatu
vinavyounda kata ya Parakuyo, kijiji hicho kilianzishwa Agosti 22 mwaka 2014
kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 301.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment