BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUPATWA KWA JUA NA MWEZI KWATIBUA MUANDAMO WA MWEZI, HIKI NDICHO KILICHOTOEA UPANDE WA WAISLAMU.


Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala, (Kulia), Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, wakitumia miwani maalum kuona tukio la kupatwa kwa jua huko Mbarali mkoani Mbeya jana Septemba 1, 2016


ASALAM ALEYKUM
TAARIFA YA MWEZI MUANDAMO WA DHUL HIJJAH MWAKA 1437H - 2016M:


Jana siku ya Alhamisi 29DHUL Qaadah 1437H sawa na Septemba mosi 2016, mwezi hakuweza kuonekana popote pale duniani kutokana na kupatwa kwa jua kwa muda mrefu kwa hivyo DHUL HIJJAH 1, 1437H itakuwa siku ya jumamosi ya septemba mwaka huu.


Siku ya ARAFAH sasa itakuwa ni siku ya jumapili ya septemba 11 2016 (9DHULHIJJAH 1437H) ambapo siku ya EIDUL ADH-AHAA itakuwa ni siku ya jumatatu septemba 12, 2016 (10DHULHIJJAH 1437H).

Tunamuomba mwenyezi mungu atufikishe katika masiku hayo adhimu na matukufu mbele ya allah na kutuwezesha kufunga masiku hayo hasa katika siku ya AARAFAAH ambayo ina ujira mkubwa sana kujalia kuingia katika Eid tukiwa tumefutiwa dhambi zetu.


Na mwenyezi mungu awakubalie ndugu zetu hijja zao na warudi kwa watu wao kwa salama wakiwa na wamesemehewa madhambi yao yote amina.

Hii ndio ratiba iliyoratibiwa na 
BARAZA LA KUFATILIA MWEZI WA POPOTE DUNIANI
Katika usiku wa kwanza wa siku kumi za kwanza za dhulhijjah... hakuna amali anazopenda Allah zaidi ya zinazofanywa katika siku kumi hizi.

Tunamuomba Allah tuweze kutekeleza barnamiji hii
1- kuhitimisha Qur'ani katika siku 9. . .yaani kuanzia usiku wa kwanza juzuu 3 kila siku

2- kuzifanyia ibada nyusiku hizi 10

3- kufunga siku 9

4- kukithirisha adhkaar na nyuradi katika hizi siku 10

5- kukariri labbaykallahumma labbayka

6- kukithirisha dua katika siku 10 hizi kwasababu dua ni bongo la ibada

7- kukithirisha kutoa sadaqa
8- kuhusisha baada ya alasiri ya siku ya arafa kwa dua
Katika amali njema, Kusali jamaa kila siku, Kusali sala ya kuchomoza jua (shuruq)

Sala ya dhuha

Kusali usiku, Usipoweza kutekeleza basi sambaza ujumbe huenda mtu akatekeleza ikaandikwa kwenye kurasa zako... na anayejulisha watu kheri ni kama aliye itenda.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: