Juma Mtanda, jphtjuma@gmail.com
Jumla ya magoli 10,876 yamefungwa na washambuliaji
22 katika mashindano ya netiboli ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 katika michezo 40.
Idadi hiyi inatokana magoli yaliyoamua ushindi yakiwa 5393 huku walinzi wa timu 11 wakiruhusu kufungwa jumla ya magoli 5483 katika michezo hiyo 40.
Idadi hiyi inatokana magoli yaliyoamua ushindi yakiwa 5393 huku walinzi wa timu 11 wakiruhusu kufungwa jumla ya magoli 5483 katika michezo hiyo 40.
Timu ya netiboli ya Uhamiaji iliibuka na ubingwa bila
kupoteza mchezo wowote baada ya kushinda michezo yote 10 na kukusanya pointi 20
ikiwa imefunga magoli 779 na kufungwa magoli 237 katika ligi hiyo iliyohusisha
jumla ya michezo 40 na kumalizika hivi karibu katika uwanja wa jamhuri mkoani
Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Mwenyekiti wa
Chaneta Tanzania, Anna Kibira alisema kuwa mashindano hayo yalishirikisha jumla
ya timu 11 ikiwa na washambuliaji 22 ambao wamefunga magoli 5393
wakati walinzi wa kila timu nao wakiruhusu kufungwa jumla magoli 5483 katika
michezo hiyo.
Kibira alisema kuwa ligi ya mwaka huu ilikuwa na
ushindani mkubwa hasa baada ya timu ya netiboli ya Polisi Morogoro kufanya
usajili wa nguvu uliopelekea Uhamiaji kushinda kombe la ligi hiyo kwa mbinde
katika mchezo wao wa mwisho uliohesabiwa kama fainali kutokana na timu hizo
kulingana pointi 18 katika michezo tisa kabla ya kukutana katika mchezo wa
mwisho na Uhamiaji kushinda.
“Ligi daraja la kwanza mwaka huu ilikuwa na ushindani
mkubwa na hii imetokana na usajili uliofanywa na timu shiriki lakini Polisi
Morogoro niwapongeze kwa kufanya usajili wa nguvu na kuleta changamoto kubwa
kwa Jeshi Stars na Uhamiaji.”alisema Kibira.
Akitaja msimamo wa ligi hiyo, Kibira alisema kuwa
Uhamiaji ndio mabingwa wa msimu wa mwaka 2016/2017 ikitetea ubingwa huo kwa
mara ya pili mfululizo huku Polisi Morogoro ikishika nafasi ya pili kwa
kukusanya pointi 18 baada ya kushinda michezo tisa na kupoteza mmoja ikiwa
imefunga magoli 659 na kufungwa 325.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Jeshi Stars yenye pointi
14 ikifunga magoli 650 ikifungwa magoli 359 na kupoteza michezo mitatu huku
Madini Arusha iliyopoteza michezo mitatu kutoa sare mchezo mmoja imeshika
nafasi ya nne na pointi 13 ikifungwa magoli 401 na kufunga magoli 531 wakati
Tumbaku Morgoro imefunga magoli 606, kufungwa magoli 457 na kupoteza michezo
minne baada ya kukusanya pointi12 ikiwa nafasi ya tano.
Polisi Arusha iliyopoteza michezo mitano imeshika
nafasi ya sita kwa kuwa na pointi 10 baada ya kufungwa magoli 523 na kufunga
magoli 512 huku Jiji Arusha yenye pointi tisa nafasi ya saba imefunga magoli
465 na kufungwa magoli 470 na sare mchezo mmoja.
Michezo mingine timu ya Kikosi cha kutengeza sare za
jeshi (CMTU) imeshika nafasi ya nane baada ya kupoteza michezo sita ikikusanya pointi
nane ikifunga magoli 447 na kufungwa magoli 452, Jiji Tanga imemaliza nafasi ya
tisa na pointi nne baada ya kushinda michezo miwili kufungwa michezo nane kwa
kufunga magoli 291 na kufungwa 646.
Ras Kagera iliyoshinda mchezo mmoja imemaliza ikiwa
na pointi mbili ikipoteza michezo tisaa ikifungwa magoli 729 ikiwa nafasi ya 10
wakati Kinondoni ya Dar Es Salaam imeburuza mkia kwa kupoteza michezo yote 10
ikifungwa magoli 794 na kufunga magoli 188.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment