BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAGUFULI KUZINDUA NDEGE MPYA ZA BOMBARDIER Q400 KESHO DAR ES SALAAM

 
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dk Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuanzia saa mbili asubuhi.

“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dk Chamuriho.mwananchi


Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: