Juma Mtanda, Morogoro-jphtjuma@gmail.com
Panzia la michezo ya ligi daraja la kwanza mchezo wa netiboli Tanzania bara 2016/2017 linafungwa leo kwa michezo minne huku wenyeji Polisi Morogoro na Uhamiaji zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa bingwa wa msimu huu mkoani hapa.
Michezo hiyo ni kati ya Madini Arusha dhidi ya Ras Kagera huku Tumbaku Morogoro ikichuana na CMTU wakati Jiji Tanga itaonyeshana kazi na Jeshi Stars na mchezo wa mwisho ni kati ya Polisi Morogoro na Uhamiaji unaosubiriwa kwa hamu kubwa kuamua ubingwa wa msimu huu.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Mwenyekiti wa chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibila alisema kuwa mchezo wa Polisi Morogoro dhidi ya Uhamiaji ndio utaotoa bingwa kutokana na timu hizo kushinda michezo tisa kati ya 10 na kukusanya pointi 18 kila mmoja.
Kibila alisema kuwa mchezo wao ni kama fainali kwani kila mmoja ameshindwa michezo yake tisa na kubakiwa na mchezo mmoja ambao unawakutanisha wenyewe na utaamua ubingwa kutokana na kulingana pointi ikitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa majira ya saa 8 mchana leo.
“Sisi chama tumeona kama mchezo baina ya Polisi Morogoro na Uhamiaji kama fainali kwani Polisi Morogoro imeonyesha kiwango bora katika ligi hii na kuipa presha ambayo nayo haijapoteza mchezo hivyo baada ya mchezo kumalizika atajulikana bingwa wa msimu huu.”alisema Kibila.
Katika michezo ya jana (Juzi) timu ya Tumbaku Morogoro ilishinda kwa ushindi mwembamba dhidi ya Jeshi Stars kwa magoli 59-54 huku Uhamiaji ikipata ushindi wa magoli 71-22 mbele ya CMTU wakati Madini Arusha iliilaza Kinondoni kwa magoli 85-5.
Polisi Morogoro ikairarua Madini Arusha kwa magoli 69-41 huku Polisi Arusha iliitambilia Jiji Tanga kwa magoli 59-30 kabla ya kupata ushindi mwingine dhidi ya mahasimu wao wa Jiji Arusha magoli 54-43 na CMTU ikiifunga Jiji Tanga magoli 65-33.
Michezo mingine Ras Kagera ilichapwa na Jiji Arusha magoli 82-35, Jeshi Stars ikaisambaratisha Kinondoni ya Dar es Salaam magoli 102-33.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment