BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KATIBU MKUU WA CUF MAALIM SEIF KUMBE HANA SABABY YA KUJIBEMBELEZA KWA RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN

 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro amesema katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif (Pichani) hana sababu ya kujibembeleza kwa Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein kwa sababu masuala ya maslahi kwa viongozi wastaafu ni ya kikatiba na kisheria na hayatolewi kwa hisani ya mtu.

Akizungumza leo kufuatia kauli ya Rais John Magufuli jana akiwa ziarani visiwani humo kwamba Dk Shein asingesaini posho na matibabu kwa ajili ya Maalim Seif kwa vile alikataa kusalimiana naye, Mtatiro alisema viongozi wastaafu wanastahili kupata matibabu na posho nyingine kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

“Tunataka kumweleza Rais Magufuli kwamba Dk Shein hana uwezo wa kufuta matibabu na posho kwa Maalim Seif kwa kuwa yapo kikatiba na kisheria,”alisema.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: