Timu ya netiboli ya Uhamiaji imetwaa ubingwa wa mashindano ya netiboli ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 baada ya kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Polisi Morogoro na kufikisha jumla ya pointi 20 uliofanyika katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Mchezo kati ya Polisi Morogoro na Uhamiaji ndio uliokuwa na taswira ya maamuzi ya kumtoa bingwa kutokana na timu kuwa kwa pointi 18 kila mmoja ikitofautiana magoli ya kufungwa na kufunga ikiwa matokea kabla ya kukutana.
Polisi Morogoro iliyomaliza ikiwa na pointi 18 ilianza mchezo kwa kasi na kuweza kuidhibiti Uhamiaji raundi ya kwanza kwa kuongoza magoli 13-12 kabla ya Uhamiaji kuibadilikia katika raundi ya pili, tatu na nne kwa kuongoza idadi ya magoli.
Raundi ya pili Uhamiaji ilipata ushindi wa magoli 24-21 dhidi ya Polisi Morogoro wakati raundi ya tatu Uhamiaji iliongeza kazi na kupata magoli 32-30 huku raundi ya nne Polisi Morogoro iliendelea kuwa mnyonge kwa kukubali tena kipigo cha kufungwa magoli 44-40 ikiwa ni tofauti ya magoli manne yaliyoamua ubingwa.
Uhamiaji ililazimika kufanya kazi ya ziada ya kuibana Polisi Morogoro kupitia kwa wachezaji wake GS, Allinafe Kamwala aliyefunga magoli 28 na GA, Zuhura Twaribu aliyefunga magoli 16 wakati Polisi Morooro GS, Mwanaidi Hassan alifunga magoli 31 huku GA, Lulu Joseph magoli 8.
Kwa upande wa uzuiaji walinzi wa timu zote za Uhamiaji na Polisi Morogoro walizuia magoli saba kila timu huku GK, Amina Jumanne alizuia magoli mawili na GD, Dolitha Mbunda magoli matano wakati wapinzani wao GK, Veronica Kikalao alizuia magoli matatu na GD, Johanri Kasika magoli manne.
Kutokana na matokeo hayo Polisi Morogoro imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 18 wakati nafasi ya tatu ilibebwa na Jeshi Stars na pointi14 huku Madini Arusha ilishika nafasi ya nne kwa pointi 14 na kukamilika nafasi ya nne bora.
Tumbaku Morogoro ilikusanya pointi 12, Polisi Arusha pointi 10, Jiji Arusha Pointi 9, Kikosi cha ushonaji was are za jeshi (CMTU) pointi 8, Jiji Taanga pointi 4, Ras Kagera pointi 2 na Kinondoni Dar es Salaam ikiburuza mkia ikiwa haina pointi kwa kufungwa michezo yote 10.
Akitangaza majina ya wachezaji bora katika nafasi mbalimbali, Kaimu mwenyekiti wa Chaneta, Zainabu Mbiro alimtaja Betina Kazinja wa timu ya Uhamiaji kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo wakati, Nasra Selemani akitajwa kuwa mfungaji bora huku, Dolitha Mbunda wa Polisi Morogoro akitwaa mlinzi bora na, Robina Thomas kutoka Jiji Arusha akiibuka kinara nafasi ya mlinzi wa kati.
Katika michezo ya kukamilisha ratiba timu ya Jeshi Stars iliweza kuibuka na ushindi wa magoli 76-34 mbele y Jiji Tanga wakati Tumbaku Morogoro ikipata ushindi wa magoli 60-5o dhidi ya CMTU na Madini Arusha ikiilaza Ras Kagera magoli 71-33.
Mashindano ya netobili ligi daraja la kwanza mwaka huu yalishikisha jumla ya timu 11 na kuanza kutimua vumbi Augost 27 ambayo yalimalizika Septemba 04 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri Morogoro.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment