BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VAZI LA TAIFA LA TANZANIA LAPEPERUSHWA NA VUMBI LA KIANGAZI ?.

 
Dodoma. Serikali imelipa kisogo vazi la Taifa na huenda mpango huo ukaachwa kama ulivyo, licha ya kuwa mchakato wake umegharimu fedha nyingi.

Kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikipigia chapuo Watanzania kuwa na vazi lao rasmi na mchakato wake ulishafika mbali kiasi cha kuundwa kwa kamati ya kushughulikia jambo hilo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameliambia Bunge kuwa mpango huo umesitishwa kwa sasa kwa kuwa Serikali iligundua kuwa inafanya mchakato wa kupata vazi la viongozi na siyo kwa Watanzania wote.

“Ni kweli tuliunda hadi kamati, lakini Serikali imegundua kuwa Tanzania ina makabila zaidi ya 120,” amesema Nape

Waziri alisema hata mataifa yanayopigiwa mfano kuwa yana vazi la Taifa hayakufanya mchakato huo kupitia serikalini, bali yalitokea kupenda vazi mojawapo na kujikuta linavaliwa na wengi.

Nape alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk Mary Mwanjelwa aliyetaka kujua kamati maalumu ya kushughulikia vazi hilo ilifikia wapi, kwani iliundwa na kufanyia kazi hadi kufikia katika nafasi nzuri ya ukamilishaji.

Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kudhibiti mavazi yasiyo na staha kwa wanamuziki wa kike nchini.

Nape amesema wizara hiyo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) imekuwa ikitoa elimu kwa wasanii kupitia vyombo vya habari, makongamano, semina na warsha juu ya umuhimu wa maadili na namna ya kubuni kazi za sanaa.

Kuhusu wasanii wanaokiuka maadili kwa kuvaa mavazi au kubuni kazi za sanaa zinazomdhalilisha mwanamke, alisema hatua za kinidhamu zinachukuliwa ikiwamo kuwafungia na kuwapa onyo kali. 


Nape alisema Sera ya Taifa ya Utadamuni ya mwaka 1997 imeelezwa kila Mtanzania ana wajibu wa kulinda mila na desturi ili kuhakikisha maadili yanalindwa na mwanamke hadhalilishwi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: