Mhe Joshua Nassari akiteta jambo Mhe Andrew Chenge.
WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya na Joshua Nassari ambao tayari wamesimamishwa kuhudhuria, huenda wakapata kifungo zaidi cha kuhudhuria vikao vya Bunge baada ya jana kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Bulaya na Nassari wanadaiwa kukiuka kanuni za uendeshaji wa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria katika Bunge la Bajeti.
Nipashe ilimshuhudia Mbunge wa Bunda Mjini, Bulaya, akiwa kwenye Ofisi za Uongozi wa Bunge akisubiri kuonana na kamati hiyo.
Alipotafutwa na Nipashe ofisini kwake jana mchana, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya, alithibitisha kuitwa kwa wabunge hao na kamati hiyo lakini hakuwa tayari kufafanua zaidi kuhusu uamuzi huo.NIPASHE
0 comments:
Post a Comment