BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATAKA RAIS WA NCHI ALIYETEMBEA NA MWANAMKE MWENYE VIRUSI VYA HIV APEWE KONDOMU


Rais wa Afrika ya Kusini, Jocob Zuma.


Naibu wa rais nchini Afrika Kusini alichukua fursa bungeni wakati ambapo rais wa taifa hilo Jacob Zuma alikuwa amesafiri nje ya nchi kuwakilisha maswala ya serikali ikiwemo kondomu isiyo na kelele na yenye ladha ya machungwa kwa wabunge.

Cyril Ramaphosa alielezea kwamba mipira hiyo ya kondomu ilitengezwa kufuatia malalamishi kwamba kondomu za serikali zilikuwa zina harufu mbaya na kelele.

Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake wakisema ''mpatie Zuma hizo''.

Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliopita wakati bwana Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.

Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini humo ambapo takriban watu milion saba wana virusi.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: