BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIWANI WA CHADEMA AKUTWA NA BUNDUKI NA DAWA ZA KULEVYA SUMBAWANGA

 
Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe.

Sumbawanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, linamshikilia Diwani wa Kata ya Izia (Chadema) na mkewe kwa tuhuma ya kukutwa na bunduki aina ya gobori na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, George Kyando amesema watuhumiwa hao wamekamatwa i dukani kwao katika eneo la soko kuu, Kata ya Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga kwenye msako uliokuwa unaendeshwa na askari wa jeshi hilo.

Taarifa za kipolisi zilieleza kuwa msako huo ulifanyika baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watuhumiwa hao wanamiliki silaha.

Kyando alisema silaha hiyo na bangi yenye uzito wa robo kilo vilikutwa vimefichwa katikati ya mifuko ya ‘sulphate’.

Amesema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na polisi walikiri kukutwa na vitu hivyo na watafikishwa mahakamani wiki ijayo baada ya upelelezi kukamilika. 


Alitoa rai kwa wananchi kuepuka kujihusisha na uhalifu na kumiliki silaha isivyo halali.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: