A,B,C TUKIO LA MKULIMA ALIYECHOMWA MKUKI MDOMONI NA KUTOKEA NYUMA YA SHINGO NA WAFUGAJI SIKU YA KRISMASI MORO
Augustino Mtitu baada ya kushonwa juzi sita katika ulimi kitengo cha meno hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG.
Juma Mtanda, Morogoro.
Mkazi wa kitongoji cha Upangwani kijiji cha Dodoma-Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa, Augostino Pius Mtitu (42) aliyenusurika kifo kufuatia kuchomwa mkuki mdomoni kisha kutokea nyuma ya shingo na wafugaji amelazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro akiuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuutoa desemba 25 mwaka huu.
Kutokana na kujeruhiwa kwa mkuki huo, Augostino Mtitu ameshonwa juzi sita katika ulimi wake huku akidumu na mkuki huo mdomoni kwa saa 6 kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa uliochukua saa moja na madaktari wa hospitali hiyo.
Majeraha hayo yamemfanya Augustino ashindwe kuongea kutokana na maumivu makali yanayomkabili ya kuathirika kwa mfupa wa taja na kuchanika kwa ulimi.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa mmoja wa ndugu wanaomuuguza, Mtitu hospitali ya mkoa huo, Stanley Andrew (41) alisema kuwa ndugu yao alikumbwa na mkasa huo majira ya saa 5 asubuhi siku ya tukio wakati akisaidia kugombelezea ugomvi uliotokana na wafugaji kudaiwa kuingiza mifugo katika shamba la mahindi la mmoja wa wakulima katika kitongoji chao.
Andrew alisema kuwa, Augostino Mtitu alichomwa mkuki huo baada ya kujeruhiwa kwa, Yohana Wisa anayedaiwa kupigwa fimbo katika ugomvi huo na kuvunjika mkono wa kulia katika mkasa uliopelekea watu tisa kupata majeraha kutokana kipigo kutoka kwa wafugaji.
“Ni mapenzi yake mwenyezi mungu ya kumfanya ndugu yetu (Augostino Mtitu) kuwa hai mpaka sasa, hebu fikilia amechomwa mkuki mdomoni na mkuki huo umekaa mdogomi kwa saa 6 kabla ya kufanyiwa upassuaji na kutoa majira ya saa 10 jioni”alisema Andrew.
Akielezea chanzo za ugomvi huo unaodaiwa kuanzishwa na wafugaji kwa kuingiza mifugo kwenyea shamba la mahindi, Andrew alisema kuwa mifugo iliingizwa kwenye shamba la, Dotto Mfaume huku, Yohana Wisa aliyekuwa jirani kuziona na kwenda kuziondoa shambani ziliendelee kula miche ya mazao.
Andrew alisema kuwa kitendo cha, Wise kutoa mifugo hiyo shambani kilisababisha ashambuliwe na wafugaji sehemu mbalimbali za mwili wake kwa fimbo uliopelekea kuumizwa kisha kupiga yowe la kuomba msaada kutoka kwa watu wa kitongoji hicho.
“Mtu wa kwanza kufika eneo la tukio alikuwa Augostino aliyemkuta, Wise akishambuliwa na wafugaji alafu akavamiwa yeye na kuchomwa mkuki mdomoni na baadaye watu waliongezeka lakini wafugaji walifanikiwa kukimbia na kuacha mifugo”alisema Andrew.
Baada ya wafugaji kuacha mifugo na kukimbia mifugo hiyo ilikamatwa na uongozi wa kitogoji lakini baadaye wafugaji wanadaiwa kurudi kufuata mifugo yao na kujeruhi watu wengine alafu kuondoka nao.
Watu wengine waliojeruhiwa katika tukio hilo ni pamoja na balozi wa serikali ya mtaa kitongoji cha Upwangaji kijiji cha Dodoma Isanga, George Andrew (65), Mwenyekiti wa Dodoma-Isanga, Stephano Luziga, Mwenyekiti wa kitongoji Upwanga, Simon Luoga, Josephati Mtitu,Paulo Thomas,Mathayo Elias na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
Mganga wa hospitali ya mkoa wa Morogoro,Dk Frank Jacob alisema kuwa desemba 25 mwaka huu, majira ya saa 10 jioni walimpokea mgonjwa, Agustino Mtitu kutoka hospitali ya wilaya ya Kilosa akiwa na mkuki mdomoni.
Dk Jacob alisema kuwa mgonjwa huo alifanyiwa upasuaji wa kutoa mkuki mdomoni na upasuaji huo ulifanyika kwa muda wa saa moja na anaendelea vizuri pamoja na matibabu mengine ya dawa.
Mganga msaidizi wa Meno hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro, Judith Mwidunda alisema kuwa baada ya Augostino Mtitu kufanyiwa upasuaji wa kutoa mkuki mdomoni juzi, leo (jana) kitengo cha meno kimemfanyia uchunguzi na kubaini kuumia mfupa wa taja la juu na ulimi kuchanika.
Judith alisema kuwa kutokana na hali hiyo wamelazimika kumchona nyuzi sita sehemu ya ulimi upande wa kulia, mdomo wa juu kuchonwa juzi nne na meno manne kufungwa nyaya maalumu.
“Tumemchona nyuzi sita katika ulimi wake baada ya kuchanika sehemu ya kulia, mdomo wa juu nao tumechona nyuzi nne lakini na meno yake manne yamekosa nguvu na kufungwa nyaya maalumu kisha itafuata kipimo cha x-rai ipigwe eneo la mdogo ili tuona pengine kama kuna athari nyingine.alisema Judith.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay) alisema kuwa serikali ifanye kazi ya kuwabaini wale wote waliohusika katika vitendo vya kinyama na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
Profesa Jay alisema kuwa ili kuweza kukomesha vitendo vya ukatili na wananchi kuchukua sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu wa amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilaya ya Kilosa.
Profesa Jay alisema kuwa matukio ya wafugaji kuvamia mashamba kisha mifugo kuharibu mazao yamekuwa mengi na pindi wakulima wanapojaribu kuondoa mifugo shambani wamekuwa wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na wengine kulazwa hospitali ya wilaya Kilosa.
“Wafugaji wamekuwa wakitumia zana za jadi kujeruhi wenzao wakulima pindi wakulima wanapojaribu kuondoa mifugo wasiendelee kuharibu mazao yao lakini kimsingi jamii hizi tunazihitaji na tunasisitiza kufuata misingi ya kuishi kwa amani”alisema Profesa Jay.
Profesa Jay alisema kuwa serikali wakati inatafuta ufumbuzi wa kudumu, inapaswa izinduke kwa kuwachukulia hatua kali kutokana na watuhumiwa baada ya kutenda makosa wamekuwa wakiranda mitaani bila wasiwasi.
“Ni tukio la juzi ndio lililonekana kuustua umma wa watanzania sijui kwa sababu ya mtu kuchomwa mkuki mdogoni lakini matukio ya wafugaji kujeruhi wakulima yamekuwa mengi karibu jimbo zima la Mikumi na wilaya ya Kilosa kiujumla”alisema Profesa Jay.
Profesa Jay alisema kuwa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kilosa limekaa na kukubaliana wafugaji wakae katika maeneo yao waliyotengewa na wakulima ili kuepusha migogoro ya ardhi lakini kufanyika zoezi la kuhakiki mifugo na kupiga chapa.
“Serikali haitumii nguvu zake za dola za kuhakikisha linakomesha migogoro ya wafugaji na wakulima na hiyo inatokana na viongozi hawatimizi wajibu wao kikamilifu na tunaomba serikali ikunjue makucha yake ili msumeno ukate huku na huku”alisema Profesa Jay.
Kwa upande wa Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alimethibitisha kutoka kwa tukio a jeshi hilo linawashikilia watu watatu.
Kamanda alisema kuwa chanzo cha mtu mmoja kuchomwa mkuki mdomoni na watu wengine kujeruhi kimetokana na wafugaji kuingiza mifugo katika shamba lenye mazao yakiwemo mahindi, maharage na miwa lakini mmilikiwa wa mifugo tayari amefahamika.
“Watuhumiwa watatu tayari wamekamatwa kutokana na mgomvi baina ya wakulina na wafugaji lakini jeshi linaendelea na msako wa watu wengine na mmilikiwa wa mifugo iliyoingia shambani amefahamika.”alisema Kamanda Matei.
0 comments:
Post a Comment