CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini, kimeshangazwa na kauli ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ya kumkejeli Rais John Magufuli kwa uamuzi wa kununua ndege.
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Arusha, Jasper Kishumbua, alihoji wakati Lowassa akiwa Waziri wa Maji na Mifugo, kushindwa kutatua tatizo sugu la maji mkoani na Wilaya ya Arumeru.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara aliyoifanya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mkoani hapa hivi karibuni.
Alisema uamuzi wa serikali kununua ndege ni mzuri na umeangalia maslahi mapana katika sekta ya usafirishaji, lakini si kiongozi aliyewahi kushika nafasi kubwa nchini ya uongozi kumkejeli Rais Magufuli.
Alisema Lowassa alipokuwa Waziri wa Maji kwanini hakutatuwa tatizo la maji mkoani Arusha hata huko wilayani Arumeru ameshindwa kupeleka maji.
Alisema CCM wilaya inamtaka Lowassa kuacha kuhubiri siasa za ulaghai huku akijua wazi kuwa kazi iliyofanywa na uongozi wa awamu ya tano ndani ya mwaka mmoja imewakuna na kukonga mioyo ya Watanzania wengi bila kujali itikadi zao na hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Alisema Majaliwa ametatua kero za wafanyabiashara ya usafiri wa Noah zinazofanya safari zake Arusha-
Namanga au Arusha-Karatu na maeneo mengine kwa kuagiza uongozi wa Mkoa kusimamia taratibu ili magari hayo yatoe huduma bora pamoja na alisisitiza watumishi wa umma kutoa huduma kwa wananchi bila kujali itikadi zao.
Alisema CCM pia imefurahishwa na jitihada za serikali kwa kuamua kurudisha eneo la Kilombero kiwanja namba 68 kilichokuwa mali ya halmashauri kwa wa machinga sambamba na kuagiza halmashauri kutowabughudhi wamiliki wa vibanda vya stendi ndogo na kubwa.
Pia Kishumbua aliwapongeza wananchi mbalimbali waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu Majaliwa alipokuwa ziarani jijini Arusha kwa sababu ya kukunwa na jitihada kubwa za kimaendeleo katika serikali ya Rais Magufuli.NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment