BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA KWENDA IKULU KUSAMKA BEN SAANANE

Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limeeleza kutoridhishwa na jitihada za Serikali za kumtafuta kada wake, Ben Saanane ambaye ametoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema wanashangazwa kuona serikali ikiweka mkazo kumtafuta 'Faru John' badala ya Saanane ambaye ana thamani kuliko mnyama huyo.

"Tunatoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa itakayowezesha kupatikana kwa Ben. Hilo likishindikana tutakwenda kumuona Rais Magufuli, Ikulu iwe kwa maandamano au utaratibu mwingine," amesema Katambi. 


Mwenyekiti huyo amefafanua kwamba Serikali haiwezi kukwepa wajibu wa kumtafuta Saanane kwa sababu ni raia wake na ana haki ya kikatiba ya kupatiwa ulinzi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: