MAJANI YA MCHAICHAI NAMNA UNAVYOWEZA KUSAFISHA FIGO ZA BINADAMU
Mchaichai unatambulika na wengi kutokana na ladha yake nzuri. Wengine wanavutiwa na muonekano wake kwa ujumla.
Lakini mchaichai ni zao la biashara ambalo halitumii dawa kama yalivyo mazao mengine kwenye kilimo chake. Hauna gharama kubwa kuukuza mpaka kuuvuna.
Licha ya mmea huo kuongezwa kwenye vyakula vingine kwa ajili ya kuleta harufu nzuri na kuongeza ladha, hutibu magonjwa.
Unatibu maradhi mengi yakiwamo homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, kadhia za ulaji wa chakula chenye sumu, maumivu ya kichwa na misuli.
Tafiti nyingi zilizowahi kufanywa zinaonyesha mmea huo una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari tumboni, mkojo na vidonda.
Mchaichai pia unatumika kama vile vinywaji mfano wa chai, kahawa au kokoa. Majani yake yakichemshwa yanatoa lishe sahihi kwa mlaji.
Kwa mtumiaji wa mara kwa mara anaweza kuzua maambukizi ya satarani.
Pia hutibu matatizo ya presha, ugonjwa wa moyo na malaria. Hufukuza mbu wakati wa usiku na inatibu mafua na baridi yabisi.
Mchaichai unasaidia mmeng’enyo wa chakula, unapunguza msongo wa mawazo, unatibu matatizo ya mifupa na kupunguza maumivu ya hedhi kwa wasichana na wanawake.
Mchaichai unaondoa taka mwilini, unapunguza unene na kuzuia maumivu ya tumbo. Unafunga kuharisha, unasafisha figo, ini, mapafu, kibofu cha mkojo na unapunguza matatizo ya UTI na unene.
Kwa wajawazito husaidia kutanua nyonga. Mafuta ya mchaichai huimarisha misuli kwa kusinga mwili.
Mafuta hayo yanatibu fangasi wa ngozi, mzio, na kutengeneza vipodozi kama sabuni na losheni. Husaidia pia kuotesha nywele kwa watu wenye kipara.
Mafuta ya mchaichai pia hutumika kwenye dawa ya kufukuza mbu. Wanaoyanywa, matone matatu kwenye kikombe cha maji, huwasidia kuondoa maradhi.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment