Tunda la stafeli lina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa hatari ukiwemo ugonjwa wa saratani na hata utafiti wa kwanza umeonyesha kuwa stakafeli lina uwezo wa stafeli wa kutibu saratani.
Utafiti huo uligundulika tangu miaka ya 1970 ilikuwa siri hadi hivi karibuni ulipowekwa bayana tena na watafiti wa masuala ya tiba za asili.
Hivi sasa wakereketwa wa tiba mbadala na dunia kwa ujumla, wanafahamu kuwa stafeli lina virutubisho vyenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya saratani kushinda hata dawa za kisasa. Tunda hili linapatikana nchini kwa wingi, mjini na vijijini. Kwa lugha za kigeni linajulikana pia kama Soursop au Graviola.
VIRUTUBISHO VILIVYOMO
Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, stafeli limesheheni idadi kubwa ya virutubisho ambavyo ni: Amino Acid, Acetogenins, Vitamin C, Iron, Riboflavin, Phosphorus, Thiamine, Calcium, Carbohydrates, Niacin na Fibers na vingine vingi.
SARATANI NA STAFELI
Ingawa suala la stafeli peke yake kutibu saratani lina mjadala, lakini hakuna shaka kabisa kuwa lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana au kupunguza makali ya saratani. Ukweli uliogundulika hivi karibuni, umewapa
wagonjwa wa saratani njia nyingine mbadala ambayo haikuwepo hapo awali. Kwani hivi sasa wanaweza kulitumia stafeli kama dawa ya kupunguza makali au kuwapa kinga dhidi ya saratani na wanaweza pia kuitumia pamoja na matibabu wanayopewa ya mionzi na kupata ahueni kubwa.
USHAHIDI WA KIMAABARA
Zaidi ya majaribio 20 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli, yamebaini haya yafuatayo:
Stafeli huua chembechembe za saratani (cancerous cells) aina 12, ikiwemo saratani ya matiti, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.
Stafeli lina mchanganyiko wenye uwezo mkubwa wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mara 10,000 zaidi ya dawa ya ‘Adriamycin’ ambayo ndiyo hutumika kutibu aina mbalimbali ya saratani.
Mchanganyiko wa virutubisho vya ‘Annonaceous’ ‘Acetogenins’ vilivyomo kwenye stafeli huua seli (cells) zilizoathirika tu na saratani, tofauti na dawa za kisasa ambazo zenyewe huua seli zilizoathirika na hata zisizoathirika.
Stafeli hudhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa, ambazo wakati mgonjwa anapozitumia, iwe zile za njia ya mionzi, sindano au vidonge, huwa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine huweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.
UMUHIMU WA STAFELI KWA WANAOTUMIA TIBA YA KISASA.
Mgonjwa wa saratani anayetumia tiba ya hospitali anashauriwa pia kula sana stafeli kwani lenyewe husaidia kupunguza makali ya dawa anazotumia.
KWA mfano baadhi ya dawa za hospitali huathiri njia ya chakula na kumsababishia mgonjwa ukosefu wa choo kwa muda mrefu, lakini stafeli likitumika hurekebisha hali hiyo na kumsaidia mgonjwa kupata choo kama kawaida.
Vilevile, baadhi ya dawa za hospitali za saratani hudhoofisha kinga ya mwili, lakini virutubisho vilivyomo kwenye stafeli, hasa vitamin C, huzifanya kinga kuwa imara na hivyo kuziimarisha hivyo kumuepusha mtu kupatwa na maambukizi mengine, kama ya njia ya mkojo, mafua na kikohozi cha mara kwa mara.
FAIDA ZINGINE ZA STAFELI NI KAMA ZIFUATAVYO:
Hutoa nafuu ya kipanda uso.
Kirutubisho aina ya Riboflavin kilichomo kwenye stafeli, husadia kutoa nafuu kwa ugonjwa wa kichwa cha kipanda usoni.
HUZUIA UGONJWA WA ANEMIA
Madini ya chuma (iron) yaliyomo kwenye stafeli, hufaa sana katika kuzuia ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia).
HUTIBU MAGONJWA YA INI
Juisi ya stafeli inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu matatizo ya kwenye ini na uvimbe kwenye kibofu cha mkojo.
HUIMARISHA MIFUPA
Stafeli ni chanzo kizuri pia cha madini ya kopa (copper) na kashiamu (calcium), virutubisho ambavyo huwa muhimu kwa ukuaji wa mifupa mwilini.
Matatizo mengine yanayoweza kudhibitiwa na stafeli ni pamoja na kuumwa miguu, maumivu kwenye ‘joints’, mwili kukosa nguvu na matatizo mengine ya viungo.
MAJANI, MIZIZI, MAGAMBA NAYO NI DAWA
Mbali ya tunda lenyewe kuwa na faida lukuki kama zilivyoanishwa hapo juu, vilivyomo vingine kwenye mti huo kama vile mizizi, majani na magamba yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali:
Unywaji wa maji yaliyotengenezwa kutokana na majani ya mstafeli hutibu magonjwa ya ngozi, chunusi na uvimbe wa mwili.
Maji ya majani ya mstafeli pia hutibu ugonjwa wa kuhara, kukohoa, kuvimba miguu, mapunye kichwani. Aidha, maji ya majani ya mstafeli yamethibitika kushusha kiwango cha sukari mwilini.
TAHADHARI
Inaelezwa kwamba stafeli linaweza kuwa siyo salama kwa wajawazito, wagonjwa wa presha ya kupanda au kushuka (hypotension or hypertension), hivyo wanashauriwa kabla ya kula, wapate ushauri wa daktari kwanza.
USHAURI
Kwa asili yake, stafeli lina kiasi kingi cha virutubisho vinavyoua bakteria, hivyo ulaji wa muda mrefu wa tunda hili kunaweza kuua bakteria wote tumboni hata wale wazuri, hivyo iwapo utalila tunda hili kwa zaidi siku 30 mfululizo, unashauriwa pia kuongezea na dawa za kulainisha njia ya chakula.
JINSI YA KULITUMIA STAFELI
Stafeli linaweza kuliwa katika aina tofauti. Kama unataka kupata faida zake zote, unaweza kulila lililoiva kama lilivyo au unaweza kutengeneza juisi yake.
Unywaji wa maji yatokanayo na majani, mizizi au magamba yake, unaweza kunywa kama chai au kinywaji kingine cha kawaida.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment