Na Juma Mtanda, Morogoro.
Watu wawili wameuawa na mmoja kujeruhiwa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kijiji cha Kisaki Stesheni na kufyatua risasi hali iliyosababisha taharuki katika katika tukio lililotokea kata ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro Vijijini majira ya saa 3 usiku jana (juzi) mkoani hapa.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, mmoja wa majeruhi aliyekimbizwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro, Juma Malekela alisema kuwa amejeruhiwa katika mkono wa kushoto katika tukio la watu wajiojulikana kurusha risasi na watu wawili kufariki dunia kutokana na majeraha.
Malekela alisema kuwa yeye baada ya kupigwa risasi alikimbizwa kituo cha afya cha Duthumi majira ya saa 6 usiku na kupata huduma ya kwanza.
“Ilipofika majira ya saa 3 usiku akiwa anauza genge lake na, Ramadhani Kayeya aliyekuwa anauza duka walisikia kelele za watu wakikimbia na kukusanyika sehemu mmoja ndipo wakatoka kuangalia kinachoendelea na baadaye walirudi ndani na muda mfupi risasi zikaanza kupigwa kabla ya wavamizi”alisema Malekela.
Wakati wa uvamizi wa tukio hilo, walimpiga risasi ambayo bahati nzuri ilipiga katika mkono wa kushoto na kuanza kutokwa damu nyingi sana kabla ya kukimbizwa kituo chapolice Kigomelo walipopewa fomu namba tatu (PF3).alisema Malekela.
“Nilikimbizwa kituo cha hospitali Duthumi majira ya saa 6 usiku na leo (jana) asbuhi nimekibizwa hapa hospitali ya mkoa ili kupigwa picha ya x-ray kuona kama kuna risasi zimenasa mwilini.”alisema Malekela.
Ramadhani Kayeya ambaye hakujeruhiwa katika tukio hilo alisema kuwa wavamizi hao walikuwa na gari ndogo aina ya Toyota Land Cruizer mbili na walipokuwa wanashambulia walipiga risasi nyingi katika eneo hilo la Kisaki Stesheni.
“Kabla ya wavamizi hao kumpiga Malekela risasi waliniuliza, kaka yako yuko wapi, lakini kabla sijawajibu nilisikia mlio wa bunduki, nilikaa chini na kujificha chini ya uvungu ndani ya duka langu na walipoondoka tu nikafunga duka,”alisema Kayeya.
Baada ya tukio kumalizika tuliona miili ya watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi huku wauaji wakiwa wamekimbia kusikojulikana.
Watu wanaodaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia ni pamoja na, Ally Hamad Mtemangani ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Bagamoyo aliyekwenda Kisaki Stesheni kwa ajili ya likizo na baada ya kufungwa kwa shule huku muingine akitajwa kuwa ni, Daudi Simoni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutokea kwa mauaji ya watu wawili wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa.
Matei alisema kuwa tayari amemtuma mkuu wa upelelezi mkoa huo kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na kubaini chanzo cha kizima cha tukio hilo.
Kamanda Matei alieleza kuwa eneo hilo la Kisaki limekuwa na matatizo ya kiusalama kutokana na madai ya kuwepo kwa watu watano wanaojiita Mungiki.
0 comments:
Post a Comment