KUFANANA KWA WAFUNGWA CHANZO CHA UGUNDUZI WA ALAMA ZA DOLE
Na Geofrey Chambua.
Mnamo mwaka 1903 mfungwa William West alifikishwa kwenye gereza la Leavenworth Penitentiary Kwenye Jimbo la Kansas Nchini Marekani Miaka 100 iliyopita.
Alipofika kwa Karani wa Masijala akaelezwa alishafungwa kwenye hilo gereza William alikataa kata kata akisema ni mara yake ya kwanza hapo, Karani akasisitiza amewahi kumuona hapo.
Baada ya kalani kueleza maelezo hayo alilazimika kupekue mafaili yake na ndipo alipomwonyesha mugshot au passport size zenye picha ya William West lakini William alistuka kuona ile picha na kusema kuwa hajawahi fungwa na hilo lilikuwa nikosa lake la Kwanza.
Baadae ikaja kugundulika kuwa kwenye gereza hilo hilo kulikuwa na mtu anaitwa Will West ambaye hana undugu wowote na William West.
Ikumbukwe wakati huo namna pekee ya kutambua wahalifu iliitwa Bertillion ambapo walipima muonekano wa mtu (physical appearance) kwa hiyo ilikua ngumu kwa kesi ya akina 'West'
Kesi hiyo ilipelekea ama ndio chanzo cha kugunduliwa kwa matumizi ya kuchukuliwa kwa chapa za mikono au (FINGERPRINTS) zinazoendelea kutumika hata hii leo.
The Strange Case of Will and William West: How Law Enforcement Learned the Importance of Fingerprinting. This bizarre story took place at the turn of the 20th century.
0 comments:
Post a Comment