TATIZO la kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi nchini, linasababishwa na kutokuwapo kwa uhusiano mzuri kati ya walimu na wanafunzi, imeelezwa.
Kadhalika, walimu wengi nchini hawafahamu changamoto zinazowakabili wanafunzi, hali inayochangia kuwapo kwa ufaulu mdogo.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Elimu ya Jamii, Solvia Temu, aliyasema hayo hivi karibuni kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, wakati akizindua utafiti wa kupima maendeleo ya elimu nchini ujulikanao kama, 'Kujipima kwa ajili ya kujifunza Afrika', utakaohusisha shule za msingi nchini.
Utafiti huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza, kwa ajili ya kufanya utafiti wa miaka mitatu katika masomo ya Hisabati katika shule zote za wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
“Lengo la utafiti huu ni kuimarisha ujifunzaji kwa wanafunzi waweze kufaulu katika masomo yao kwa kuwaelekeza walimu mbinu mbalimbali za kuwafundisha,” alisema.
Alisema walimu wengi wanashindwa kuwawezesha wanafunzi kufaulu kwa sababu hawajui changamoto zinazowakabili pamoja na kukosa mbinu za kuwafundisha.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza Elimu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Prof. Joe Lugalla, alisema mazingira yanayotatiza wanafunzi kushindwa kusoma na kufaulu vizuri, ni uhaba wa majengo, tatizo la maji, upungufu wa walimu wenye uwezo na kutokuwapo kwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu na wanafunzi.
Alisema moja ya mambo watakayofanya ni kuwafundisha walimu mbinu za kuwafundisha watoto na kwamba mradi huo utahusisha Chuo cha Ualimu Vikindu, walimu na maofisa elimu wa Temeke.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ SIRI YA WANAFUNZI KUSHUKA UFAULU KUINGIA SEKONDARI YAANIKWA HADHARANI, WALIMU WAMO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment