BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA MAWENZI MARKET FC MORO YAPIGA HESABU KALI KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA 2017/2018

Kikosi cha klabu ya Mawenzi Market FC Morogoro.
 

Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya soka ya Mawenzi Market FC imeanza kuweka mikakati kabambe ikiwemo kuendeleza kasi yao ya uchezaji kwa kuhamishia kwenye michezo ya hatua ya nne bora ya ligi daraja la pili Tanzania bara (SDL) ili kuwa moja ya timu zitakazofuzu kuinga ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa katika mahojiano maalumu, Kocha mkuu wa Mawenzi Market FC, Hussein Mao alisema kuwa anamshukuru mwenyezi mungu kwa kuiwezesha timu yao kumaliza hatua ya awali na kuibuka kinara katika kundi B kwa kukusaanya alama 23.

Mau alisemaa kuwa kufuzu kwao kuingia kwenye hatua ya nne bora kunawafanya kuingia kwenye michezo hiyo kwa kasi zaidi baada ya kuilaza Namungo FC katika mchezo wa mwisho wa bao 1-0 ugenini.

Kitu kinachohitajika kwa sasa ni kuendeleza mshikamano, umoja na upendo ili kutimiza malengo kuiwezesha Mawenzi Market FC kuwa moja ya timu tatu za kuingia na kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.alisema Mau.

“Tumemaliza hatua ya kwanza Mawenzi Market FC tukiwa vinara kwa kumaliza na pointi 23 hivyo tunaingia kwenye awamu ya pili ya michezo ya nne bora tukiwa na nguvu lakini inatupasa kuwa makini zaidi kupambana kufa na kupona kuhakikisha tunasimama imara na kutwaa nafasi moja kati ya timu tatu zitakazofuzu.”alisema Mau.

Mau alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa Mawenzi Market FC kufikia hatua kama sio wachezaji, benchi la ufundi, mashabiki na wadau kujidhatiti kwa hali na mali kuisaidia timu katika michezo ya hatua ya kwanza.

“Tunahitaji ushirikiano mkubwa uliotuwezesha sisi (Mawenzi Market) hatua ya kwanza kuongoza kundi letu na ushirikiano huo sasa tuuhamishia katika michezo ya hatua ya pili ya fainali ya michezo ya nne bora na hilo linawezekana kwani umoja ni nguvu.

Wakati Mawenzi Market FC ikiweka mikakati ya kucheza hatua ya nne bora na kupiga hesabu za kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao, ndugu zao timu ya Sabasaba United FC yenyewe imejikuta ikiangukia pua baada ya kuaga ligi daraja la pili kufuatia kumaliza na pointi saba na kuburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo.

Sabasaba United inayomikiwa na wafanyabiashara wa kuuza nguo ilijikuta ikiaga ligi hiyo kwa kukubali kutandikwa bao 2-1 na The Might Elephant FC ya Songea katika mchezo wao wa mwisho uwanja wa jamhuri Morogoro.

Ushindi huo wa The Might Elephant dhidi ya Sabasaba United umeifanya ufikisha pointi 20 huku Namungo FC ya Lindi ikimaliza na pointi 14.

Mkoa wa Morogoro una timu moja ya ligi kuu Tanzania bara Mtibwa Sugar wakati ligi daraja la kwanza ikiwakirishwa na Polisi Morogoro huku ligi daraja la pili Tanzania bara kukiwa na timu nne ikiwemo Burkina FC, Mkamba Rangers, Sabasaba United FC na Mawenzi Market FC.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: