RAIS MAGUFULI AMTEUA LUTENI JENERALI MABEYO KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA
Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange.
Rais John Pombe Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akichukua mahala pake jenerali Davis Mwamunyange aliyestaafu.
Taarifa kutoka ikulu iliotumwa katika vyombo vya habari inasema kuwa Luteni huyo sasa amepandishwa cheo na kuwa jenerali kamili.
Mkuu mpya wa majeshi nchini Tanzania Jenerali Venance Mabeyo
Magufuli: Sijazima demokrasia Tanzania
Wakati huohuo rais amemteua meja jenerali James Mwakibolwa kuwa mnadhimu mkuu wa majeshi ya ulinzi akichukua mahala pake Jenerali Mabeyo.Pia yeye alipandishwa cheo cha luteni jenerali.
Rais amesema kuwa uteuzi huo unaanza kutekelezwa mara moja.Tarehe ya kuapishwa kwa wawili hao itatangazwa baadaye
0 comments:
Post a Comment