Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kumteua waziri mpya wa habari na michezo.
Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Bw Nape Moses Nnauye ndiye aliyekuwa anashikilia wadhifa huo.
Aidha, Dkt Magufuli amemteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Dkt Mwakyembe amekuwa akihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria.
"Uteuzi huu unaanza mara moja," taarifa kutoka ikulu imesema.
Wateule wote wataapishwa Alhamisi kwa mujibu wa ikulu.
Bw Nauye amevuliwa majukumu yake siku moja baada yake kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu uvamizi uliotekelezwa na mtu anayedaiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika studio za kituo cha habari cha kibinafsi cha Clouds mwishoni mwa wiki. Waziri wa zamani wa habari aliyevuliwa madaraka Nape Nnauye
Kamati hiyo, kwenye ripoti yake, ilionekana kumkosoa Bw Makonda na kusema alitumia vibaya mamlaka yake.
Kamati hiyo ilipendekeza, miongoni mwa mengine, kwamba Bw Nnauye awasilishe malalamiko ya waandishi wa habari dhidi ya mkuu huyo wa mkoa kwa Rais wa Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya polisi waliongia na silaha za moto kwenye chombo hicho cha utangazaji.
Akipokea ripoti hiyo, Bw Nnauye pamoja na kuwataka viongozi wa umma kufanya kazi kwa uweledi, aliahidi kukabidhi taarifa hiyo kwa mamlaka za juu zaidi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kutokana na mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo.
Dkt Magufuli ameonekana kufurahishwa na utendakazi wa Bw Makonda na mara kwa mara amesifu hatua alizochukua.
Rais John Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelee kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye rais wa nchi. Dkt. Harrison George Mwakyembe awali alikuwa waziri wa sheria sasa ni waziri wa habari
Dkt Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Prof Kabudi, ambaye ameteuliwa kuwa waziri mpya wa katiba na sheria aliteuliwa Januari mwaka huu kuwa mbunge mteule. Awali Prof. Palamagamba Aidan Kabudi alikuwa mhadhiri wa chuo kukuu cha Dar es salaam na sasa ameteuliwa kuwa waziri wa sheria
Yeye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria na alikuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Joseph Warioba.BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ BAADA YA WAZIRI NAPE NNAUYE KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI HIKI NDICHO KILICHOFUATA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment