Dar es Salaam. Rais John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya katika Baraza la Mawaziri kwa kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye anakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyokuwa ikishikiliwa na Nape Nnauye.
Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa kesho mchana.
0 comments:
Post a Comment