Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande.
Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Barcelona FC imefuzu hatua ya pili ya ligi daraja la nne Manispaa ya Morogoro 2016/2017 kwa kishindo hatua ya 16 bora baada ya kutembeza vipigo mfululizo kwa wapinzani wake iliyopelekea kukusanya pointi 13 katika michezo mitano na kumalizika kinara kundi lake katika ligi hiyo mkoani hapa.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande alisema kuwa Barcelona FC imekuwa moja mwa timu 16 zilizofuzu kutinga hatua ya pili ya ligi daraja la nne hatua ya 16 bora.
Maharagande alisema kuwa Barcelona FC ilifanikiwa kupata ushindi katika michezo minne kati ya michezo mitano baada ya kutembeza vipigo dhidi ya wapinzani wake na kutoa sare mchezo mmoja.
Barcelona FC ilianza kupata ushindi wake wa kwanza kuifunga Majengo Mapya FC bao 2-0 huku Liti FC ikitandikwa 1-0 kabla ya Kingaru United kuambulia sare ya bao 1-1 wakati Shooting Star ilikung’utwa bao 3-1 na Mlunda FC ikipata kipigo cha bao 2-0 na kukusanya pointi 13 katika mzunguko huo wa awali.
Maharagande alizitaja timu nyingine zilizofuzu kuwa ni Beach Boys FC iliyovuna poiniti 11, Hot Star FC pointi 10 huku Kihonda Maghorofani FC ikiwa na pointi nane.
“Ligi yetu kwa sasa zipo katika mapumziko ya wiki moja na kutokana na mapumziko haya timu zimeruhusiwa kufanya usajili ili kuongeza nguvu katika vikosi vyao kwa ajili mzunguko wa hatua ya pili ya ligi hii.”alisema Maharagande.
Nyingine ni Young Star FC yenye poiniti 9, Jakalanda United pointi 9, Kihonda United pointi nane, Chipolopolo FC pointi 15, Chicago FC pointi 12 na Dawa yao Sport Club pointi tisa.
Timu ya Home Boys FC ilimaliza na 11, Moro City FC pointi 10, Sultan Rangers pointi saba, Liti FC 11 na Shooting Star pointi nane.alisema Maharagande.
Maharagande alisema kuwa ligi hiyo ilianza kutimua vumbi Desemba 28 mwaka 2016 na kumaliza hatua ya awali Marchi 19 mwaka huu ambapo kuna mapumziko madogo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment