BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

GUANTANAMO BAY GEREZA LA WAFUNGWA WATUKUTU NA LENYE ULINZI MKALI ZAIDI DUNIANI


Guantanamo Bay au Hori ya Guantanamo (kwa Kihispania Bahía de Guantánamo) ni hori ya Bahari ya Karibia inayoingia kusini mwa kisiwa cha Kuba yenye upana wa km 20 na urefu wa km 8.

Eneo hili lilikodishwa na Kuba kwa Marekani mwaka 1903 kwa muda wa miaka 99. Wakati ule Kuba ilitwaliwa na wanajeshi Wamarekani baada ya Vita ya Marekani dhidi Hispania ya 1898.


 Marekani ilidai kibali cha Kuba kwa utawala kwake juu ya Guantanamo Bay kama sharti kabla ya kuondoa jeshi lake.
Kwa sababu hiyo serikali ya Kuba ya mapinduzi ya 1958 haikutambua tena mapatano haya kwa sababu inadai Kuba ililazimishwa kijeshi kukubali.

Marekani imejenga bandari ya kijeshi pamoja na uwanja wa ndege na huwa na kikosi cha askari 9,500. Kuna ukuta na fensi ya kutenganisha kituo na maeneo chini ya serikali ya Kuba.

Tangu mwaka 2001 kambi la wafungwa limejengwa kituoni lenye mnamno wafungwa 1,000 hasa kutoka Afghanistan waliokamatwa baada ya mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani na vita katika Afghanistan iliyofuata. Marekani ilipeleka hapa watu waliokamatwa Afghanistan na penginepo duniani wanaoshtakiwa kuwa magaidi wa Al-Qaida au Taliban lakini ambao hawakuwa bado na kesi mbele ya mahakama.

Utaratibu huu ni nje ya sheria za Marekani na haulingani na sheria za kimataifa kuhusu kuwatendea wafungwa wa vitani.
Nchi nyingi duniani zimepinga kuwepo kwa makambi haya na kudai wafungwa watendewe ama kama wafungwa wa vita au kupelekwa mahakamani kama magaidi.


Mwaka 2007 ni bado zaidi ya wafungwa 500 kambini.

Rais Barack Obama alikuwa aliapa kuwa angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo. Hata hivyo Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani la Guantanamo Bay, Cuba.

Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni "watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena". Kwa sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao. 


Bw Trump alikuwa amepinga mpango wa Obama wa kufunga jela hiyo tangu wakati wa kampeni.

Mwezi Februari alisema: "Asubuhi hii, nimemtazama Rais Obama akiongea kuhusu Gitmo, sawa, Guantanamo Bay, ambayo kusema kweli, ambayo kusema kweli, hatutaifunga.
"Tuaicha iendelee kutumika... na tutawarundika watu wale wabaya huko, niamini mimi, tutawaweka watu wengi huko."
Mnamo 17 Desemba, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Pentagon inapanga kuwahamisha wafungwa wengine 17 siku chache zijazo.

Rais Obama ameidhinisha kuhamishwa kwa wafungwa lakini Bunge la Congress ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican limewekwa masharti mengi.


Bunge hilo linaitaka wizara ya ulinzi kutoa taarifa kuthibitisha viwango vya kiusalama vimetimishwa angalau siku 30 kabla ya hatua kama hiyo kuchukuliwa.

Nchi kadha zimewapokea wafungwa wa zamani wa Guantanamo, zikiwemo Ghana, Senegal, Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE), Uganda na Cape Verde.


Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. 50 kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru.

Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya mashambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia "wapiganaji maadui".
Gereza hilo hugharimu Marekani $445m (£316m) kila mwaka na ni moja ya magereza yenye gharama za juu sana nchini Marekani.


(Each Guantanamo prisoner costs US taxpayers roughly $800,000 a year, which is more than 30 times as expensive as housing a prisoner on domestic soil)

Yasemekana ujenzi wa Gereza hilo umetumia Teknolojia ya hali ya juu sana kiasi ambacho wahandisi wengi mahiri duniani wameshindwa kuijua ramani yake kamili

Wafungwa wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana.


Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009. Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa mashtaka.

Ghana imetoa idhini kwa wawili hao kukaa nchini huko kwa miaka miwili, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ghana Hanna Tetteh amesema.


Kwa mujibu wa stakabadhi za jeshi la Marekani, Mahmoud Omar Bin Atef ni raia wa Yemen aliyezaliwa Saudi Arabia mwaka 1979 . Alikamatwa nchini Afghanistan 2001.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: