HUYU NDIYE RAIS ALIYEFUNGWA MIAKA 25 JELA
Alberto Fujimori alikua Rais wa 62 wa nchi ya Peru iliopo Amerika kusini Mashariki, aliongoza Peru kutoka mwaka 1990- 2000, Peru haikua imara kiuchumi, vuguvugu la mtikisiko wake kisiasa lilianza mwaka 1997.
Mwaka 1997 gazeti moja jipya na maarufu sana nchini Peru la caretas lililoripoti uraia wa Alberto Fujimori kwamba Alberto Fujimori alizaliwa katika mji wa Kawachi Kumamoto nchini Japan.
Alberto alikuwa ana uraia wa nchi mbili yaani Japan na Peru ambapo taarifa kutoka Serikali ya japan ilieleza wazazi wa Fujimori walimzaa Alberto nchini Japan na wazazi wake walihamia nchini Peru wakiwa na watoto wawili akiwemo Alberto.
Lakini rais huyo alikuja kupata kashfa ya rushwa na uvunjaji na ukiukwaji wa haki za binaadamu.
Na Geofrey Chambua.Mwaka 2000 alipata kashfa ya rushwa na uvunjaji wa haki za binadamu hivyo mwaka 2000 alikimbilia Japan, akiwa japan alijaribu kujiuzulu urais wa Peru kwa kutumia mawasiliano ya njia ya Fax, bunge la congress la Republican nchini Peru lilikataa kujiuzulu kwa Rais huyo akiwa nje ya nchi mpaka arudi nchini Peru ili apigiwe kura ya kutokua na imani nae ili kuendelea kupewa heshima.
Rais Fujimori alisafiri kutoka Japan kwenda nchini Chile ndipo alipokamatwa alikuwa bado ni Rais na kesi yake ilirindima kwa muda mrefu, ndipo mwaka 2007 alihukumiwa miaka 5 baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya rushwa.
Mwaka 2009 mamlaka ya Peru alisomewa mashtaka ya uvunjaji wa haki za binaadamu nchini nchini Peru na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kwenda jela miaka 25.
0 comments:
Post a Comment