BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA MAWENZI MARKET FC YAMTIMUA KOCHA MKUU MOROGORO

Kipa wa klabu ya Transity Camp ya Shinyanga, Edson William akiondosha hatari langoni kwake huku akizongwa na wachezaji wa Mawenzi Market FC wakati wa mchezo wa ligi daraja la pili hatua ya nne bora kusaka timu tatu za kufuzu kuingia ligi daraja la kwanza msimu ujao kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo kwenye mchezo huo Transity Camp ilikung'utwa bao 2-0.
 
Juma Mtanda, Morogoro.

Kocha mkuu wa klabu ya Mawenzi Market FC Morogoro, Hussein Mau amefungashiwa virago baada ya kutimuliwa kukinoa kikosi hicho kilichopo kwenye ligi daraja la pili Tanzania bara (SDL) hatua ya nne bora ya kusaka timu tatu za kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Mlezi wa klabu hiyo, Afred Katabarura alisema kuwa klabu hiyo imeachana na kocha mkuu, Hussein Mau na msaidizi wake, Buya Kassim kutokana na madai ya utovu wa nidhamu na kuigawa timu.

Katabarura alisema kuwa klabu hiyo imelazimika kuwatimua makaocha hao na kumsaka kocha mwingine wa kumalizia michezo iliyobakia ili kutimiza ndoto za kutinga ligi daaraja la kwanza msimu ujao.

“Mipango yetu Mawenzi Market FC ni kucheza ligi daraja la kwanza lakini tunahitaji kupata ushindi katika michezo yetu miwili iliyobakia ili kumaliza na pointin 12 kujihakikishia moja ya nafasi tatu za kufuzu kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.”alisema Katabarura.

Katabarura alisema kuwa klabu hiyo inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya ligi hiyo na hulazimika kutembeza bakuri kuomba fedha kwa wadau mbalimbali ili kuiwezesha timu kusafiri.

“Ili timu iweze kusafiri nje ya Morogoro kucheza michezo yake inalazimika kuwa na bajeti kati ya sh800,000 hadi sh900,000 hivyo kuifanya klabu kumudu gharama za maandalizi ya timu.”alisema Katabarura.

Kwa upande wa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Hussein Mau alieleza kuwa alikabidhiwa timu ya Mawenzi Market FC ikiwa na pointi tano katika ligi daraja la pili hatua ya makundi na kuiwezesha kumaliza vinara wa kundi lao ikiwa na pointi 20.

“Nilikabidhiwa timu ikiwa na pointi tano lakini kama kocha mkuu nilipambana na kumaliza kundi letu tukiwa vinara kwa kuongoza kwa pointi 20 iliyotuwezesha kuingia kwenye hatua ya nne bora ya kusaka timu tatu za kufuzu kucheza ligi daraja la kwanza.”alisema Mau. 


Akielezea juu ya kutupiwa virago kuifundisha klabu hiyo, Mau alisema kuwa yeye hawezi kushangaa madai hayo lakini ni jambo la kushangaza mbona timu imekuwa ikifanya vizuri tangu amekabidhiwa kuinoa ?.alihoji.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: