BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WIMBO WA NEY WA MITEGO WAFUNGULIWA....SASA RUKSA KUPIGWA VITUO VYOTE VYA REDIO NA TV


NEY WA MITEGO.

Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe ameagiza msanii aliyekamatwa kuhusiana na wimbo wake alioutoa hivi karibuni aachiliwe huru.

Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania

Nay wa Mitego hata hivyo ametakiwa auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.

Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.

Mapema leo, Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania (Basata), lilikuwa limetangaza kuufungia wimbo huo kwa jina Wapo usichezwe kwenye vyombo vya habari au kutumika kwa namna yoyote ile.

"Basata linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za sanaa, hata kufikisha ujumbe mbalimbali wa kufundisha, kuelimisha, kuburudisha na hata kuonya," taarifa kutoka kwa baraza hilo ilisema.

"Baraza linawaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi (na) hatua kali zitachukuliwa juu yao."

Awali kulikuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli alikuwa ameagiza wimbo huo uendelee kuchezwa.

Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe hata hivyo alionekana kukerwa na taarifa hizo.

Bw Kabwe alisema Rais hana mamlaka yoyote ya kuamua wimbo uchezwe au usichwezwe.

"Ilikuwa ni makosa kumkamata Nay na agizo la Rais halina maana pia," aliandika kwenye Twitter.

WIMBO WAPO WA...NEY WA MITEGO.
Verse 1:
Unachokipanda leo ndicho utachovuna kesho.
Imeandikwa Mwanaume kula kwa jasho.
Najiuliza hivi ni nani kaiona kesho.
Chapa mwendo na ukilala hauna chako.
Hivi uhuru wa kuongea kwenye hii nchi bado upo?.
Usije kuongea vitu kesho ukajikuta sentro.

Chorus:
Kuna viongozi wavuta bangi? "wapo "
Maana wana maamuzi ya kise.... "wapo"
Kuna walio mmiss Jakaya? "wapo"
Walio choka kuisoma namba? "wapo"
Kuna walio poteza malinda? "wapo"
Kuna wasanii mateja? "wapo"
Kuna mademu wanasagana? "wapo"
Kuna vidume wanalelewa? "wapo"
Kuna wasanii wanarogana? "wapo"

Verse 2
Kuna Radio na Tv, naona zimeshapoteza CV.
Hakuna uhuru wa habari, wala taarifa ya habari.
Wanapindisha pindisha tu kuiogopa serikali.
Siamini nchi inaendeshwa na kiki.
Siasa inafunika mziki.
Viongozi wanashindana kukiki.
Wanagombea front page, wauze kwenye gazeti.
Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti.

Verse 3
Kiongozi mwenye busara anapokea ushauri.
Anapokea mawazo,haweki mbele kiburi.
Hey! Samahani mheshimiwa, hivi unamjua BASHITE?.
hili ni jipu jipya toka koromije.
Limesha iva na usaa, limeshatunga.
Na kukabidhi sindano ya kulidunga.
Daktari haogopi ukubwa wa kidonda.
We_si Dr wa majipu, tumbua hakuna kuvunga.
Kuvamia ofisi za watu kumbe nayo ni kazi.
Hakuna noma wanangu pigeni kazi.
Boda boda kazi, bajaji Kazi.
Eti! Vipi? Kukaba nayo kazi?.
Refa ni wao piga manati.
Vita ya Masai na mmang'ati.
Biashara ya ngono na Super shafti.
Pumzi imekata nashika shati...

Hahahahahaha! Wewe mtu gani sasa......
Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa......
Umerongwa wewe,........
unajiona ndugu yake na Yesu ee....
Oya! Wanangu eeeh! Round hii mtanyooka haki ya Mungu.
Naona kichaa kapewa Rungu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: