BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Mwarobaini namna unavyotumika kufukuza wadudu katika shamba

Mti wa mwarobaini unaweza kutumika katika njia tatu au zaidi katika utengenezaji wa viuatilifu. Njia hizo ni majani na punje zake na maji, majani na maji ya moto na majani na mkojo wa ng’ombe

Majani ya mwarobaini, punje na maji

Njia hii hutumia majani tu ya mwarobaini pamoja na punje za mwarobaini ambavyo kwa pamoja huchanganywa na maji na kisha kuachwa kwa siku saba.

Vifaa: Andaa mifuko ya safleti kama saba. Hii ni ile ya ujazo wa kilo 25. Andaa majani ya mwarobaini na punje za mwarobaini. Andaa mapipa ya lita 200 kama saba, maji na vifaa vya kumwagilia.

Jinsi ya kuandaa
1.Toboa mifuko ya saflet matundu madogo madogo

2.Chukua majani na punje za mwarobaini kisha kwa pamoja weka katika mifuko ya saflet ya kilo 25.

3. Jaza maji katika matanki ya lita 200.

4.Chukua mfuko wa saflet kisha weka majani na punje husika ndani ya mfuko kisha tumbukiza ndani ya matanki ya lita 200.

5.Funga vizuri mfuko wenye majani na punje ili usizame. Utauacha kwa muda wa wiki moja au siku saba kisha utaondoa mfuko wa saflet na maji yatakuwa yashabadilika rangi na kuwa na harufu kali tayari kwa matumizi

Jinsi ya kuitumia
Anza umwagiliaji kama kawaida wakati wa asubuhi kwa muda wa saa moja. Weka dawa hiyo kwenye majani na udongo. Njia hii inaweza kutumika wiki nzima au kwa siku tatu mpaka nne kwa wiki. Ukiwa na shamba kubwa utakahitajika kuwa na matanki mengi

Majani ya mwarobaini na maji ya moto

Dawa nyingine ni Majani ya mwarobaini na maji ya moto. Dawa hii inafanya kazi vizuri na inachukua muda mfupi kuiandaa.

Ili kutengeneza utahitaji kuwa na Majani ya mwarobaini kwa kiwango cha ukubwa wa shamba lako, maji, sufuria na jiko. Chukua majani ya mwarobaini kisha chemsha jikoni kwa muda wa dakika 10 mpaka 20. 


Mara baada ya maji kubadilika rangi hakikisha hayachemki sana kwani maji yatapungua. Baada ya hapo utaepua na kuweka katika chombo kingine kwa ajili ya kuweka shambani. 

Dawa hii huwekwa kwenye mmea ulioathiriwa na wadudu au hata mme usioathirika kwa ajili ya kinga.Ondoa Majani yaliyoathirika na weka dawa hii mara tatu au mara nne kwa wiki.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: