Dar es Salaam. Timu ya Tanzania, ‘Taifa Stars imeifunga Botswana mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Mabao ya Mbwana Samatta yalitosha kuwafuta machozi mashabiki wa soka nchini baada ya kufunga dakika ya 2 na 87 katika mchezo huo.
Botswana walifanya mashambulizi kadhaa katika dakika ya 22 na 27 na kufanikiwa kupata kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda. Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe. Pia aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye alizua shangwe uwanjani hapo alipoingia na kuwapungia mkono mashabiki.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ SAMATTA AIMALIZA BOTSWANA WAKATI STARS IKIPATA USHINDI WA 2-0 UWANJA WA TAIFA DAR
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment