SERIKALI YASHINDWA KUPATA FEDHA ZA MKOPO NJE YA NCHI
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
Dodoma. Serikali imeshindwa kupata fedha za mkopo wa nje yenye masharti ya kibiashara katika bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na hali ya soko la fedha la kimataifa kutokuwa nzuri hasa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huo wa fedha.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo bungeni jana wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali.
Amesema kuwa katika mwaka huo wa fedha Serikali ilipanga kukopa katika vyanzo vya kibiashara Sh2100.9 bilioni ili kugharamia miradi ya maendeleo nchini.
“Katika kipindi hicho riba ilipanda kutoka wastani wa asilimia sita hadi asilimia tisa. Kutokana na sababu hiyo Serikali iliahirisha mchakato wa kukopa kutoka kwenye masoko hayo,”amesema. Hata hivyo, amesema gharama ya ukopaji katika masoko ya ulaya imeanza kuimarika.Mwananchi
0 comments:
Post a Comment