BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI AVUNJA SHERIA WAKATI AKIENDESHA GARI


Waziri wa polisi nchini Australia anasema kuwa hakujua kwamba alikuwa akivunja sheria wakati alipochukua simu yake akiwa anaendesha gari lake.

Troy Grant, mbunge mpya wa South Wales alichukua picha na kuichapisha katika ujumbe wa Twitter alipokuwa nyumbani.

Baada ya kuambiwa makosa yake ,bwana Grant alijiwasilisha katika kituo cha polisi ambapo alipigwa faini ya dola 250.

''Hii inawakumbusha watu kwamba hakuna mtu aliyejuu ya sheria ,alisema Grant''.

Waziri huyo alisimamishwa barabarani wakati alipopiga picha gari moja lililokuwa likibeba kondoo mbele yake.

''Sikujua kwamba kile nilichokuwa nikifanya kilikuwa kinyume cha sheria, bwana Grant alisema siku ya Jumanne''.

''Hili ni funzo kwangu, na natumai ni swala ambalo jamii inachukua funzo''.

Chini ya sheria hiyo ,madereva wanaweza kutumia simu bila kuishika.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: