YAANGA YAICHEFUA POLISI DODOMA BAADA YA KUGOMA KUCHEZAN NAO MCHEZO WA KIFARIKI
LICHA ya sababu zilizoelezwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa kwamba sababu za kushindwa kwao kuja makao makuu imetokana na uchovu pamoja na kubana kwa ratiba ya michezo kwa klabu hiyo, uongozi wa timu ya Polisi Dodoma umelalamika kupata hasara.
Katibu wa Polisi, Michael Mtebene alisema; "Tulishakamilisha utaratibu wote kuelekea mchezo huo maalumu wa kirafiki ikiwa ni pamoja na kuhifadhi sehemu watakayofikia kwa malazi ambayo tulishalipia kiasi cha gharama hivyo kutokuja kwao kunamaanisha tumepata hasara huku nasi tulishakuwa kambini kujiandaa na mchezo huo."
Yanga ilikuwa kucheza mechi hiyo, lakini kutokana na kukabiliwa na ratiba ngumu ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na mchujo wa Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa klabu hiyo umeamua kuichomolea Polisi dakika za jioni.
0 comments:
Post a Comment