BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AUAWA KWA KUFUGA NG'OMBE WA MAZIWA


Muislamu mmoja nchini India amefariki kutokana na majeraha aliopata baada ya kundi moja la wanaume waliokuwa wakisafirisha ng'ombe kushambuliwa na wanachama wa kundi moja linalodaiwa kulinda ng'ombe.

Kulingana na ripota wa BBC Nitin Srivastava aliyesafiri hadi katika kijiji cha mwathiriwa cha Jimbo la kaskazini la Haryana, wanakijiji walikuwa wakipigania kumuona kijana huyo aliyetoka hospitalini.

Azmat ambaye hutumia jina moja pekee amejifunika nguo , huku akiwa na jeraha la mbavu, damu katika jicho lake la kushoto mbali na majeraha ya kushambuka katika mikono yake na tumbo.

Hatahivyo ana bahati ya kuwa hai.

Azmat pamoja na watu wengine wanne walishambuliwa na walinda ng'ombe wakati walipokuwa wakisafirisha ng'ombe walizonunua kutoka Jaipur katika jimbo la kaskazini la Rajasthan wakielekea katika shamba lao la ng'ombe wa maziwa huko Hiryana.Ng'ombe zinadaiwa kuwa takatifu nchini India

Licha ya kuwa na vibali halali walitolewa katika barabara kupigwa na fimbo huku umma ukitaka wachomwe wakiwa hai.

''Iwapo polisi hawangefika na kutuokoa sote tungekuwa tumefariki ,aliambia BBC Hindi''.

Ngombe hutambulika kuwa mnyama mtakatifu na raia wa dini ya Hindu walio wengi na kwamba mauaji ya ngombe ni haramu katika majimbo mengi ya India.

Mwezi uliopita ,jimbo la Gujarat lilipitisha sheria inayoharamisha uchinjaji wa ng'ombe na kwamba wanaopatikana wakifanya hivyo watapewa kifungo cha maisha
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: