KUOGA KWA MAJI YA MOTO NI SAWA NA KUFANYA MAZOEZI KWA SAA NZIMA!
Na Geofrey Chambua.
Watu wengi hupendelea kuoga kwa maji ya moto ili kuepusha maradhi ya kifua wakati wa msimu wa baridi kali lakini kuna faida nyingine ya kiafya inayopatikana kuoga kwa kutumia maji hayo hivi karibuni Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Loughborough wamegundua kuoga kwa maji ya moto ni sawa na kufanya mazoezi kwa saa limoja.
Kwa mujibu wa Utafiti huo faida za kiafya kama kupunguza kiasi cha sukari mwilini husaidia mwili kutengeneza homoni inayojulikana kama Metabolism inayosaidia mwili kupungua.
Ili kukamilisha utafiti huu watu 40 walitumika kwa kuoga kwenye maji ya moto yenye sentigredi 40 na wote walionekana kupunguza Mafuta (Calories) 140 ambayo ni sawa na kukimbia kwa saa moja.
Utafiti huu pia umesema kua kuoga kwa maji ya moto kunasaidia kuimarisha mfumo wa upumuaji, kukuepusha na shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari.
Nyongeza
Faid ya kuoga maji ya moto ni pamoja na kuusaidi katika kuyeyusha mafuta yanayojigandisha mwilini baada ya jasho kuktoka mchana kutwa.
Pia yanasaidia katika kuufanya mwili ujisikie fresh yani ni kama maasage fulani hivi ya maji, maji ya baridi sanasana huwa ni muhimu kwa kuchangamsha mwili lakini pia mahospitalini huwashauri wagonjwa wenye homa kali kuoga maji ya baridi ili kushusha hiyo homa kwa njia ya maji kwanza
0 comments:
Post a Comment