BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUOGELEA UTUPU NI KINGA KIAFYA NA TIBA

KUOGELEA ni sehemu ya starehe ya umma na mazoezi ya kiafya,ambayo katika upande wa pili wa shilingi inasimama katika swali kama ina athari zozote kwa watu?

Utafutaji wa majibu yake umesimama katika mtazamo unaozaa swali jingine, la kupata uainisho wa athari hizo zenye sura mtambuka na kuzaa mitihani na mjadala mrefu.

Ni dhana inayoangusha mtihani katika hoja ya usalama wa kiafya, kisaikolojia, kijamii na kisheria ulioko kwenye suala la kama mtu anaogelea akiwa amejisitiri na nguo au vinginevyo, uhalali uko upande upi?

Katika baadhi ya sehemu za nchi mbalimbali, kuna maeneo kunakoruhusiwa watu kuogelea wakiwa ‘watupu.

Hata hivyo, mjadala wa ama watu waogolee watupu au la una mzizi mirefu wa kipindi zaidi ya karne moja iliyopita.

Tangu kuingia karne ya 20, mjadala na uwepo kuongelea bila ya mavazi yanayomsitiri muogeleaji umechachamaa zaidi, huku katika nchi kama Marekani kukizua mjadala mkali wa kijamii.

Huko ni katika taifa ambako kwenye majimbo tofauti, kuna sheria zinapishana, tayari kuna maeneo ambako ni ‘ruksa’ kisheria kuogelea ‘mtupu.’

Inaelezwa kuwa katika baadhi ya nchi kama vile Uingereza na Canada, hakuna sheria za kuzuia, hiyari ya kutovaa nguo.

MAONI YA MADAKTARI

Wataalamu wa tiba na afya wana maoni yao kuhusu mantiki ya mjadala huo. Mmojawapo ni Dk. Lance Brown wa jijini New York, Marekani anayefafanua kuwa:
”Kuvaa nguo za kujisitiri kunamuongezea jasho mwogeleaji na mtu kupata upele na muwasho. Ipe ngozi nafasi ya kupumua.”

Wataalamu wanasema, kitendo cha kuwa ‘mtupu’ kinaipa ngozi nafasi ya kupata Vitamini D kirahisi.

Mshauri nasaha wa mambo ya jinsia, Shaun Galanos anasema kuwa ni suala ambalo linapendeza kuanzia chumbani, hadi juani katika mandhari ya kuogelea.

"Kuwa mtupu’ si kwamba inakuongezea vitamin D pekee, hata hisia zako,” anasema na kuongeza:” Inasaidia hata mzunguko wako (wa damu)na kuondoa sumu katika damu.”

Watafiti wa afya wanasema kuwa mwili wa binadamu hupokea vitamini D kwa wingi unapoanikwa juani, hata walau kwa wastani wa kati ya dakika 10 hadi 15.

Mtaalamu Dk. Jenn Mann, anachangia mada zaidi akisema kuwa watu wasiishie kuendekeza mlo tu, wakati kuna mbadala mzuri wa kuota jua.

"Kutumia muda wako ukiwa ‘mtupu’ juani ni namna ya kuwasiliana na mwili wako. Watu wengi hivi sasa wanajiweka mbali na suala la kuipa hisia mwili, ambayo inaweza kumsaidia.

Dk. Mann anaenda mbali zaidi, akiwashauri kinamama (na hasa wenye ngozi” nyeupe kutumia njia hiyo kama mbadala wa kujipodoa,akiamini inawasaidia.

Kuna madai kwamba zipo aina za ushahidi unaothibitisha maisha ya kuogelea bila ya nguo, vivyo hivyo mtu kuwa ‘utupu’ anapokuwa faragha kama vile chumbani imewasaidia watu.

Hoja hiyo inadai namna walivyonufaika watu hao inahusu mengi, kama vile kupata hewa safi na kumjengea ngozi mwororo.

Kisaikolojia, pia inaelezwa kuwa ni tendo linalomuondolea mtu hata hofu na msongo wa mawazo unaotokea kwa wakati huo na mtu anajihisi kuwa huru zaidi, akipigwa na upepo.

Pia, inaelezwa kuwepo hoja kwamba wengi sasa wanaunga mkono mtazamo huo wa kuogelea kuwa watupu katika baadhi ya maeneo, ili kunufaika hivyo kiafya.

SABABU ZA KITAALAMU

Miongoni mwa yanayochambuliwa na wataalamu kwa mtazamo wa muhtasari wa misingi ya kiafya, inahoji:

•Kwa nini tuna utamaduni wa kuvaa nguo, ilhali tuajua tunaenda kulowesha nguo zetu?

•Ngozi tupu inakauka haraka zaidi kuliko ikifunikwa na nguo.
•Kuwa ‘mtupu’ mbele ya wenzako kunajenga mazingira ya wenzako kujifunza kwako mwenye tabia hiyo ya kutovaa nguo, namna ulivyo ambavyo mwili wenye afya njema.

•Pia, inafafanuliwa kwamba mtu anapoingia kuogelea bila ya kuwa na mavazi, inamnusuru mwogeleaji na athari za muwasho na mengine kwenye ngozi kutoka katika mavazi ya kuogelea.

Kinachofafanuliwa ni kwamba, inakuwa rahisi kwa mwogeleaji kutambua mara moja kwa macho na hisia kasoro au chochote kibaya katika ngozi na mwili wake, hata kitambi kinapoanza, hali inayomsaidia kuchukua hatua.

•Utafiti wa kisayansi hivi karibuni, unaonyesha kuwa namna mtu anavyokuwa ‘mtupu’ mbele ya kundi la watu, anakuwa na nafasi ya kutathmini vyema mwili wake na uhalisia wa kiafya anaopaswa kuwa nao.

Wataalamu wa afya wanashauri watu kuondokana na dhana ya kuona haya kukaa bila ya nguo katika baadhi ya maeneo wanayoruhusiwa, wakijiamini kwenye tendo hilo.

Je, katika jamii ya nchini na Afrika kwa jumla, inatekelezeka? L Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa taarifa mbalimbali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: