POLISI WATEMBEZA KIPIGO KWA WAUMINI WAKIWA KANISANI NA KUUA MMOJA
Ubalozi wa Marekani nchini Sudan umeukashifu vikali uvamizi wa polisi kwa kanisa moja katika jiji kuu la Khartoum, ambapo mtu mmoja aliuliwa kufuatia mzozo wa ardhi.
Mtu mwingine alijeruhiwa na 13 kutiwa mbaroni katika tukio hilo la tarehe 3 Aprili.
Wafuasi wa kanisa hilo walikuwa wamekaa kidete kwa wiki mbili wakati polisi walishambulia majengo hayo.
Taarifa kutoka kwa Ubalozi wa Marekani ilitaja shambulizi hilo kuwa la unyama na ikasema kuwa wametamaushwa pakubwa na tukio hilo katika shule ya Omdurman Evangelical na Omdurman kanisa Presbyterian
Ilisema kuwa hatua hiyo ya polisi ilihusishwa na utata wa ardhi na mwekezaji binafsi aliyedai alikuwa amenunua majengo hayo.
Kanisa hilo ambalo linaendesha shughuli za shule hiyo, lilianzishwa na wamishenari kutoka Amerika mwaka wa 1924.
0 comments:
Post a Comment