BAADHI ya wabunge wametaja sababu za kuanguka kwa watoto wa viongozi wa serikali katika uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA), kuwa ni pamoja kuchoshwa kuwachagua kwa historia ya wazazi wao.
Watoto hao wa viongozi wa zamani na waasisi wa Taifa ni Makongoro Nyerere ambaye alipata kura 81 na Zainab Kawawa aliyeambulia kura 137 kati ya 334 za wabunge waliokuwa bungeni wakati wa uchaguzi huo.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na Nipashe katika viwanja vya bunge jana, walisema kuanguka kwa watoto hao wa viongozi kumetokana na wabunge kuchoshwa na hali ya kuwachagua kwa ukubwa wa majina ya wazazi wao.
Walidai kuwa wamekuwa wakipewa kura nyingi lakini hawana uwezo wa kutumikia nafasi hizo.
Mmoja wa wabunge hao (jina linahifadhiwa), pia alisema walishindwa kujieleza ipasavyo kama ilivyo kwa wagombea wengine kwenye kinyang’anyiro hicho.
Awali walipokuwa wakijieleza, Zainab ambaye ni mtoto wa Hayati Rashidi Kawawa, alionekana kujikanyaga katika maelezo yake huku akidai kuwa kulikuwa na kelele bungeni.
Kwa upande wa Makongoro ambaye ni mtoto wa Rais wa serikali ya awamu ya kwanza, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alipokuwa akijieleza na kuomba kura, alitumia muda wake kuwasalimia wabunge na kutamka ‘shikamoo’ kwa kila mtu bila kujali umri na jinsia.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ SIRI YA WATOTO WA VIGOGO KUDONDOKEA PUA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI NDILO HILI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment