Hata hivyo wakati likizo hiyo kubwa takatifu ya kiislamu inapowadia, wengi wa waislamu bilioni 1.8 huwa na matumaini kwa ishara ya kushiriki sherehe hizo.
Waislamu hufuata kalenda inayoambatana na mwezi.
Waislamu hufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan na kujizuia kula chakula na kunywa kuanzia asubuhi hadi jioni.
Ikiwa mwezi kiislamu ingefuata na kalenda ya jua, watu amabao wanaishi sehemu fulani za dunia wangesherehekea Ramadan yao msimu ya joto huku wakiwa na siku ndefu ya jua huku sehemu zingine za dunia zikiwa na vipindi vifupi vya misimu ya baridi.
Lakini ndani ya dini ya kiislamu kuna mdahalo kuhusu ni lini sherehe hizo zinastahili kuanza.
Waislamu kwenye nchi nyingi hutegemea habari kuhusu kuonekana kwa mwezi mpya badala ya kuangalia anganiawao wenyewe.
Wengine hufuatilia kalenda ya mwezi, huku wengie nao wakifuatilia sayansi ya angani kutangaza kuonekana kwa mwezi mpya.
Kwa hivo tarehe za Eid hutofautiana kote duniani, licha ya kuwepo tofauti ya siku moja au mbili hivi.
Kwa mfano mamlaka nchini Saudi Arabia, yenye waislamu wengi wa Sunni, hutangaza kumalizika mwezi wa Ramadan, kutokana na maoni ya watu ambao huona mwezi mpya.
Kisha waislamu kwenye nchi zingine hufuata mkondo huo.
Lakini nchini Iran yenye waislamu wengi wa Shia hutegemea matangazo ya serikali.
0 comments:
Post a Comment