Tume ya Maendeleo ya Ushirika imesema mafisadi wote waliotafuna fedha za vyama vya ushirika watafikishwa mahakamani na kufilisiwa mali zao bila kujali ni lini waliiba fedha hizo.
Naibu Mrajisi wa Udhibiti wa tume hiyo, Collins Nyakunga amesema hata kama walifanya uhalifu huo miaka 20 iliyopita, wafahamu kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Nyakunga amesema wizi wa mali za vyama vya ushirika unaofanywa na baadhi ya watendaji imekuwa changamoto ya maendeleo ya vyama hicho.
Naibu huyo ametoa kauli hiyo wakati Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) likitangaza maadhimisho ya 19 ya siku ya ushirika duniani yatakayofanyika Julai Mosi,mkoani Dodoma.
“Changamoto hii tumeanza kukabiliana nayo, hata kama uliiba fedha kwenye vyama vya ushirika miaka 20 iliyopita ni suala la muda tu tutakukamata na kukufikisha mahakamani,”amesema na kuongeza: “Vyama vya ushirika si shamba la bibi kwamba kila mtu anaruhusiwa kuvuna.”
Mwenyekiti wa Bodi ya TFC, Renatha Mwageni amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kwa umma kuhusu ushirika.
Amesema wakati Tanzania ikitarajia kufanya maadhimisho hayo, taifa linakabiliwa na tatizo la ajira. “Tuna tatizo la ajira, tatizo la masoko na pembejeo za kilimo kwa wazalishaji, changamoto hizi zinaweza kutatuliwa kupitia biashara na mfumo wa ushirika,” amesema.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment