TASWIRA YA SWALA YA EID EL FITR VIWANJA VYA ISLAMIC FAUNDATION MOROGORO JUNI 25/2017
Sheikhe Yahaya Hussein kutoka mkoa wa Arusha akihutubia umati wa waumini wa dini ya kiislamu wakati wa swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Islamic Foundation Manispaa ya Morogoro leo, waumini wa dini ya kiislamu huswali swala la Eid El Fitr duniani kote baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani. PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG.
Sheikh Abdallah Makoo (Wa pili kutoka kushoto) akiwa amejumuika na waumuni wa dini ya kiislamu wakati wakifuatilia mawaidha kutoka kwa Sheikhe Yahaya Hussein (Hayupo Pichani) katika swala ya Eid El Fitr.
Nasoro Kassimu Kisalala na Meneja wa kituo cha Redio na Imaan TV Morogoro, Kassim Limo (Mwenye koti) wakiwa katika ibada ya swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Islamic Foundation baada ya kumalizkka kwa funga ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mtoto Abdullatif Salum (4) akijumuisha na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Islamic Foundation katika Manispaa ya Morogoro.
Waumini hao wakisudu wakati wa swala hiyo ikiwa moja ya njia ya kunyesha unyenyekevu mbele za mwenyezi mungu.
Waumini hao wakitawanyika katika viwanja vya Islamic Foundation Manispaa ya Morogoro baada ya swala ya Eid El Fitr kumalizika wakirejea manyumbani kusherehekea sikukuu hiyo.
0 comments:
Post a Comment