Mchezaji wa tenisi anayeorodheshwa nambari miongoni mwa wanawake Serena Williams amepiga picha za utupu katika kurasa ya kwanza ya jarida la August Vanity Fair.
Nyota huyo wa tenisi alibaini kwamba alikuwa akitarajia mwanawe wa kwanza na mpenziwe Alexis Ohanian kabla ya michezo ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Aliambia jarida hilo kwamba hakutarajia chochote hadi alipobaini kwamba alikuwa mgonjwa wakati wa mazoezi.
Picha ya utupu ya Serena katika jarida la vanity fair
Lakini rafikiye alishuku kwamba huenda ni mjamzito na kuamua kuchukua vipimo.
Serena alifanya vipimo hivyo wakati alipokuwa akipigwa picha na kampuni moja ndani ya Hoteli moja nchini Australia na kusema kuwa alipigwa na butwaa wakati alipopata majibu.
''Mungu wangu, hii haiwezekani- ni lazima nicheze mchuano mmoja'',alisema. Nitacheza vipi mashindano ya Australian. Nilikuwa nimepanga kushinda taji la Wimbledon mwaka huu''.Serena Wiliams na mpenzi wake Alexis Ohanian.
Rafikiye Jessica baadaye alitumwa kununua vifaa vyengine vitano vya kupima uja uzito ili kumthibitishia Serena kwamba ni mjamzito.
Vipimo vyote vilithibitisha.Habari hiyo pia ilisema vile Serena na mpenziwe walivyokutana 2015.
Alimchumbia Disemba katika meza hiyo hiyo ya Cavalieri katika hoteli moja huko Italy ambapo walikutana.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kimataifa /
michezo /
slider
/ MCHEZAJI TENISI SERENA WILLIAMS APIGA PICHA ZA UTUPU AKIWA NA MIMBA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment