BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WAWILI WAPIGWA RISASI KATIKA KIJIJI CHA MANGWI KIBITI


Kibiti. Viongozi wawili wamepigwa risasi katika Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).

Waliopigwa risasi wametajwa kuwa ni mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa tukio hilo.

Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi. Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: