IGP AWATAKA ASKARI KUSHIRIKIANA VYEMA NA WANANCHI
IGP Simon Sirro.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefungua majengo mawili ya ofi ya usalama barabarani na la michezo huku akiwahimiza askari wa jeshi hilo Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya kufanya kazi kwa weledi, kuwa waadilifu, kujituma na kuwa na mahusiano na kushirikiana na wananchi katika ulinzi wa taifa na kupambana na uhalifu.
Aidha, imefahamika kuwa madereva 12,280 wamekamatwa kati ya Januari hadi Juni mwaka huu katika makosa mbalimbali ya usalama barabarani na kutozwa faini ya Sh milioni 368.4.
Akizungumza na askari hao wa Polisi wa Tarime/ Rorya jana katika hafla ya uzinduzi wa majengo hayo yaliyojengwa kwa gharama zaidi ya Sh milioni 40.
Kamanda wa Polisi wa Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe alisema majengo hayo yamegharimu Sh 21,978,000, wakati jengo la michezo ambalo halijakamilika linatarajiwa kukamilika kwa zaidi ya Sh milioni 25.
Alizitaja changamoto nyingine zinazokabili Kikosi cha Usalama Barabarani ni gari, pikipiki za kufanya doria ili kudhibiti vitendo vya makosa ya barabarani.
0 comments:
Post a Comment